Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Manchester United wamekubali kutoa pauni milioni 59.7 kumsajili Angel Di Maria kutoka Real Madrid, na kuvunja rekodi ya uhamisho ya Uingereza.Angel Di Maria alipotembelea uwanja wa mazoezi wa Manchester United, Carrington jana jioni kabla ya kukamilisha uhamisho wake kutoka Real Madrid kwa pauni milioni 59.7
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina, 26, yuko mjini Manchester na atafanya vipimo vya afya siku ya Jumanne, kabla ya kukamilisha uhamisho ambao, ukithibitishwa utafikisha pauni milioni 132 zilizotolewa na Manchester United msimu huu kusajili wachezaji.
Huenda Di Maria akacheza mechi yake ya kwanza dhidi ya Burnley siku ya Jumamosi, mchezo wa ligi kuu.
Ada hiyo itazidi rekodi ya uhamisho ya Uingereza ya pauni milioni 50 zilizotolewa na Chelsea kumchukua Fernando Torres kutoka Liverpool mwaka 2011.
Manchester United mara ya mwisho walivunja rekodi ya Uingereza ya uhamisho mwaka 2002 walipotoa pauni milioni 29.1 kumsajili Rio Ferdinand kutoka Leeds United.
Bonyeza Hapa

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top