Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Leo Agosti 27,2014,Usiku, Arsenal wanatinga Uwanjani kwao Emirates kurudiana na Klabu ya Uturuki Besiktas kwenye Mechi ya Raundi ya Mwisho ya Mchujo ya UEFA CHAMPIONZ LIGI 2014/2015.

 Wiki iliyopita huko Instanbul, Besiktas na Arsenal zilitoka 0-0 na Arsenal wanahitaji ushindi tu ili kufuzu kwani Sare yeyote ya Magoli itamaanisha Besiktas ndio wataingia hatua ya Makundi ya UEFA CHAMPIONZ LIGI ambayo Droo yake itafanyika huko Monaco Siku ya Alhamisi Agosti 28,2014.

Arsenal wanaingia kwenye Mechi hii bila ya Kiungo wao mahiri Aaron Ramsey ambae alipewa Kadi Nyekundu kwenye Mechi ya Kwanza huko Instanbul.

Pia Arsenal itamkosa Nahodha wao Mikel Arteta mwenye tatizo la Enka na vile vile kumkosa Straika wao Olivier Giroud ambae pia ameumia Enka.

Kukosekana kwa Giroud kunaweza kutoa namba kwa Chipukizi Yaya Sanogo au Lukas Podolski au hata Alexis Sanchez kuchezeshwa kama Sentafowadi au ikibidi, Arsene Wenger kumtumia Joel Campbell.

Wakati Besiktas wana Kikosi kamili na Straika wao Demba Ba yu tayari kurejea tena Jijini London kuitesa Arsenal kama alivyokuwa akifanya akiwa na Klabu yake ya zamani Chelsea, Klabu hiyo ya Uturuki itakuwa bila ya Meneja wao kutoka Croatia kwenye Benchi, Slaven Bilić, ambae alipewa Kadi Nyekundu katika Mechi ya Kwanza na hivyo kulazimika kukaa Jukwaani kwa Mechi hii.
Bonyeza Hapa
**Mechi zote kuanza Saa 3 Dakika 45 Usiku**Ratiba zote za mechi ya leo hapa chini na muda wake 




Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
27 Aug 2014

Post a Comment

 
Top