Kwa
mujibu wa daily mail hizi ni picha za kwanza za mabaki ya ndege ya Air
Algerie ambayo ilianguka mashariki mwa nchi ya Mali ikitokea Ouagadougou
Burkina faso kuelekea Algiers Algeria.
Kwenye eneo la ajali hii iliyoua watu wote 116 waliokuwemo ndani
baada ya kupoteza mawasiliano dakika 50 baada ya kupaa, kumepatikana
mabaki ya ndege yenyewe pamoja na mabaki ya baadhi ya viungo vya
binadamu.
Ajali hii inakamilisha hesabu ya ajali kubwa ya tatu ya ndege kutokea
ndani ya kipindi cha siku saba huku nyingine zikiwa ni ajali za ndege
ya Malaysia Ukraine na nyingine ya TransAsia Airways iliyotokea Taiwan na kuua watu 48.
Wafaransa
51, 27 wa Burkina Faso, Walebanon nane, Waalgeria sita, Wacanada watano
na Wajerumani wanne ni miongoni mwa abiria waliokuwemo kwenye hii
ndege huku wengine wakiwa ndugu kama inavyoonekana kwenye baadhi ya
picha hapa chini.
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WHATSAPP 0712-483 331
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu bonyza hapa
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro




















Post a Comment
Post a Comment