Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati alipokuwa mgeni rasmi kukabidhi Tuzo za washindi wa mashindano ya kuhifadhi qur-aan, yaliyofanyika leo Julai 20, 2014, kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi, mshindi wa pili wa mashindano ya kuhifadhi Qur-an, ambaye ni Mtanzania, Said Omary Said, wakati wa hafla ya hitimisho la mashindano hayo iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, leo Julai 20, 2014. Wa pili kushoto ni Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi, mshindi wa kwanza wa mashindano ya kuhifadhi Qur-an, Hatham Sadar, kutoka nchini Kenya wakati wa hafla ya hitimisho la mashindano hayo iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, leo Julai 20, 2014. Wa pili kushoto ni Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi na baadhi ya viongozi wakiwa katika picha ya pamoja na washindi watatu wa mashindano hayo baada ya kukabidhiwa zawadi zao.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi na baadhi ya viongozi wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mashindano hayo baada ya kukabidhiwa zawadi zao.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi na baadhi ya viongozi wakiwa katika picha ya pamoja na washindi watatu na majaji wa mashindano hayo baada ya zoezi la kukabidhi zawadi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya waumini wa dini ya Kiislam, wakati akiondoka kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee baada ya kukabidhi zawadi za washindi wa mashindano ya kuhifadhi Qur-an, yaliyomalizika leo Julai 20, 2014, jijini Dar es Salaam. Picha na OMR
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WHATSAPP 0712-483 331
 
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu bonyza hapa
 

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top