Hizi
ni stori ambazo ukizisikia unaweza kushtuka kuona mtu anawezaje,sasa
Unaambiwa kutoka katika mahakama kuu jijini Eldoret Nchini Kenya kuna
mwanamke aliamua kuvua nguo ili kupinga uamuzi wa jaji kwenye kesi
yake.Kesi iliyokuwa ikimkabili mwanamke huyo ilikua ikuhusu mzozo wa
ardhi dhidi yake na mwanamke mwingine ambapo wawili hao waliripotiwa
kuoana na kwa mujibu wa desturi na mila za jamii ya wa Nandi inamruhusu
mke kumuoa mke mwingine.Mila hiyo huwa inazingatiwa endapo mwanamke
aliyeolewa ameshindwa kupata watoto au kubainika kuwa tasa na pengine
anahitaji kuendeleza kizazi katika familia aliyoolewa,hivyo mwanamke
anayeolewa na mke mwingine haruhusiwi kua na uhusiano na mke aliyemuoa
bali atatafuta mume atakaye zaa naye watoto.
Kwenye
kesi Hakimu Silah Munyao alikubaliana na hoja ya mlalamishi kuwa
hakukua na ndoa na akatoa ruhusa ya kutimuliwa kwa mshtakiwa Hellen Tum
[mkewe Tapkili Metto]kutoka kwa shamba hilo na kufidhiwa.
Kwenye
kesi ya za iliyowasilishwa mahakamani mwaka wa 2005,Tum alikua
amemshtaki mumewe Tapkili Metto kwa kumkana licha ya kuishi naye kama
mume na mke tangu mwaka 1989.
Hata
hivyo Tapkili alikataa kuoana na Tum, Akiongeza kwamba yeye alikua
msaidizi wa nyumba tu yaani Housegirl,hakimu munyao amesema hajaridhika
na mashtaka kwa upande wa mshtakiwa kwamba watoto ambao Tum alimzalia
Tapkili kwa kua hakukua na yeyote alisema alishuhudia ndoa baina ya wake
hao wawili.
Muda
mfupi baada ya uamuzi wa mahakama Bii Tum alivua nguo nje ya mahakama
huku akimtukana hakimu kwa sauti ya juu kabla ya wapita njia kumtaka
atulie.
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro








Post a Comment
Post a Comment