Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This



Jeshi la polisi mkoani Iringa limetumia mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi ambao walivamia na kuanza kuchota mafuta kwenye lori la kubeba mafuta baada ya kupata ajali. 
 
Ajali hiyo imetokea jana eneo la msitu wa serikali wa Saohil wilayani Mufindi kwenye barabara kuu ya Iringa –Mbeya ambapo watu wawili walijeruhiwa kwenye ajali hiyo.
 
Polisi wamelazimika kutumia mabomu kuwatawanya wananchi hao ambao walikuwa wakiendelea kumiminika kutaka kuiba mafuta kwenye lori hilo ili kuwaepusha na hatari ambayo ingeweza kutokea kama lori hilo lingeshika moto.
 
Mashuhuda wamesema chanzo cha ajali hiyo ni kupasuka kwa tairi ya mbele ya lori la mizigo lililokuwa linatokea mkoani Mbeya na hivyo kukosa mwelekeo na kuligonga gari la kubeba mafuta lililokuwa linatokea mkoani Iringa na kuanguka.
 

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top