MKAZI
wa Kimara Amina Ibrahim (27), amepandishwa Kizimbani katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kinondoni Jijini Dar es Salaam akikabiliwa na shitaka la
kumuua mtoto wa kambo.
Akisomewa
kosa hilo leo mbele ya Hakimu Amalia Mushi, Wakili wa Serikali Faustine
Sylivester, alidai kuwa tukio hilo lilitokea Juni 18 mwaka huu huko
Kimara, Wilayani hapo.
Sylivester alidai kuwa
mshitakiwa alikuwa akiishi naye na ndipo alipoamua kumuua mtoto huyo
ajulikanaye kwa jina la Munir Dodi (6), wakati akifahamu kuwa kufanya
hivyo ni kosa la jinai kufanya hivyo kwa mujibu wa sheria za Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.
Mshtakiwa hakutakiwa kujibu
kitu chochote kutokana na kosa lake kwani Mahakama hiyo haina uwezo wa
kusikiliza kesi hiyo, hivyo kesi imeahirishwa hadi Agosti 15 mwaka huu
itakapokuja kwa ajili ya kutajwa.
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro








Post a Comment
Post a Comment