
Takriban
watu 15 wameuawa na wengine 200 kujeruhiwa vibaya baada ya majeshi ya
Israeli kulipua shule inayoendeshwa na Umoja wa Mataifa kuwahifadhi
wakimbizi wa ndani kwa ndani wanaotoroka mashambulizi ya Isareli katika
ukanda wa Gaza .
Wizara
ya Afya katika ukanda wa Gaza imedhibitisha shambulizi hilo katika
shule hiyo iliyoko Beit Hanoun ambayo inatumiwa kama makazi ya wakambizi
wapalestina wanaotoroka makombora ya Israili.
Shambulizi
hilo ni la nne kutokea katika vituo vinavyomilikiwa na Umoja wa Mataifa
tangu Israeli ivamie ukanda huo yapata majuma mawili yaliyopita.
Kufikia sasa Wapalestina 725 wameuawa .

Waisraeli 30 wameuawa wengi wao wakiwa ni wanajeshi katika siku 16 za makabiliano kati ya Israeli na Hamas.
Israeli iliishambulia Gaza Julai tarehe 8 ikitafuta mbinu za kuzima mashambulizi ya makombora ya Hamas yanayotokea Gaza.
Awali
mwsimamizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia maswala ya
Misaada bi Valerie Amos alisema kuwa hali ya maisha imeendelea kuzorota
katika ukanda huo na kuwa kuna haja ya dharura ya kusitishwa kwa vita
ilikufanikisha utoaji wa misaada ya kibinadamu .
Bi
Amos alisema kuwa watu laki moja(118,000) wanaishi katika kambi za umoja
wa mataifa zilizoanzishwa katika shule zinazoendeshwa na UN.

Mkuu huyo wa UN alisema kuwa maji yamepungua na chakula pia hakitoshi kuwalisha wakimbizi hao wote .
Bi Amos amesema kuwa asilimia 44% ya Gaza hapakaliki kwa Wapalestina.
Hayo
yamejiri baada ya Waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu amesema kuwa
anasikitikia vifo vya Wapalestina lakini wajibu unamtegemea kiongozi wa
Hamas ambaye bado anashikilia kuwa Israeli hainabudi kukoma kuikalia
Gaza kimabavu.
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WHATSAPP 0712-483 331
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu bonyza hapa
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment