Habari ya mchungaji huyo iliandikwa na gazeti hili lenye uthubutu wa kuanika maovu bila kujali mhusika ana cheo gani, wiki mbili zilizopita ikiwa na kichwa ‘HEE! BABA MCHUNGAJI!’
Katika habari hiyo ilielezwa kwamba baba mchungaji huyo alikuwa akitaka kuvunja amri ya sita na mke huyo wa mtu baada ya mwanamke huyo kwenda kanisani hapo kupata maombi maalum ya deliverance ili apate mtoto.
Ilidaiwa kwamba mara baada ya waumini au kondoo wake kuona picha na habari ya baba mchungaji huyo gazetini walisusa kwenda kanisani hapo.
Habari zilizonaswa kutoka kanisani hapo kutoka kwa muunini mmoja (jina linahifadhiwa) zilidai kuwa baba mchungaji huyo ameingia mitini na hajulikani alipo.
“Ilikuwa ni aibu kubwa sana kwa mtumishi wa Mungu. Baada ya gazeti kuwa mitaani baba mchungaji hajaonekana tena na kanisa limefungwa,” alisema mmoja wa waumini hao bila kujua kuwa anazungumza na OFM
>>>>>>>GPL
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WHATSAPP 0712-483 331
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu bonyza hapa
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment