Jerryson
Tegere baada ya kuongezewa mkataba na timu yake ya Yanga amewasili
mazoezini leo. (Picha na ukurasa wa Facebook wa Yanga sc).
Nizar Khalfan (kushoto) alikuwepo katika mazoezi hayo .
Kazi na dawa, baada ya mazoezi, wachezaji wakaanza kupunga upepo
Nizar Khalfan (kushoto) hana masihara, anatafuta pumzi kali ya msimu ujao.
MAKAMU
bingwa wa ligi kuu soka Tanzania bara, klabu ya Yanga ya Dar es salaam
imeanza mazoezi ya kujiwinda na msimu wa 2014/2015 wa ligi kuu na kombe
la Kagame katika Fukwe za Coco Beach jijini Dar es salaam.
Mazoezi
hayo yapo chini ya kocha wa makipa, Juma Pondamali `Mensah` wakati huu
klabu ikimsubiri kocha mpya, Mbrazil, Marcio Maximo ambaye anatarajia
kuwasili kesho kama mambo yatakwenda kama yalivyangwa.
Mazungumzo
ya Maximo na Yanga sc yalisimamiwa na bosi mwenyewe, Yufus Manji, hivyo
kwa asilimia nyingi, Mbrazil huyo mwenye heshima zaidi nchini Tanzania
kutokana na mafanikio aliyoyapata wakati akiifundisha Taifa stars atatu
kukinoa kikosi hicho chenye masikani yake mtaa wa Jangwani kariokoo
jijini Dar es salaam.
Wakati
Yanga wakiendelea kumsubiri Maximo, tayari aliyekuwa kocha msaidizi,
Charles Boniface Mkwasa ameshaondoka na kuelekea Uarabuni.
Mkwasa
amepata kazi nchini Saudi Arabia na taarifa zilibainisha kuwa ameenda
kuungana na aliyekuwa bosi wake Yanga, kocha mholanzi, Hans Van der
Pluijm alitetimka kwa makubaliano baada ya mkataba wake kumalizika
mwishoni mwa msimu uliopita.
Yanga imeweza kuweka wazi majina ya awali ya baadhi ya wachezaji ambao hawataitumikia klabu hiyo msimu ujao wa ligi kuu.
Msimu
uliopita Yanga ilikuwa na kikosi cha wachezaji 30 kutoka timu ya
Wakubwa na wachezaji watano (5) kutoka timu ya vijana (U20) waliokuwa
wamepandishwa kwa ajili kupata uzoefu na kuiongozea nguvu timu ya
wakubwa katika michezo mbalimbali.
Hata
hivyo kutokana na ripoti ya benchi la ufundi iliyowasilishwa mara baada
ya ligi kumalizika, wachezaji 11 wameachwa katika usajili na tayari
uongozi umemalizikana nao na kuwa huru kutafuta timu nyingine.
Wachezaji
hao ni: David Luhende, Athuman Idd "Chuji", Geroge Banda -U20, Yusuph
Abdul -U20, Rehani Kibingu -U20, Hamisi Thabiti, Reliants
Lusajo, Bakari Masoud - U20, Shaban Kondo, Abdalllah Mguhi "Messi"
U-20 na Ibrahim Job .
Yanga imewaongezea
mikataba ya miaka miwili miwili wachezaji wake Jerryson John Tegete,
Said Bahanuzi, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Ally Mustapha `Barthez`, Mbuyu
Twite, Juma Abdul, Oscar Joshua, Simon Msuva.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro








Post a Comment
Post a Comment