Mahakama nchini Misri
imewahukumu jela kifocngo cha kati ya miaka saba na kumi wandishi watatu
wa habari wa shirika la habari la Al Jazeera waliokuwa wamezuiliwa kwa
miezi sita nchini humo.

Greste na watuhumiwa wenzake wakiwa wanasubiri hukumu yao
Mwenzake Baher Mohamed alifungwa jela miaka kumi.
Watuhumiwa wengine kumi na moja waliohukumiwa bila ya wao kuwepo gerezani, walipokea vifungo vya miaka 10 kila mmoja.
Hukumu ilipotolewa, Greste kwa hasira aligonga
mkono wake katika eneo ambako walikuwa wamezuiliwa huku mwenzake
akibururwa kutoka mahakamani na walinzi wa gerezani.
Wandishi watatu wa Al Jazeera wamefungwa miaka 7 jela kwa kueneza habari za kupotosha
Familia za watuhumiwa nao wakaangua kilio. Kesi
hii imelaaniwa sana kote duniani hasa na mashirika ya kutetea haki za
binadamu pamoja na mashirika ya habari ya kimataifa.
Lakini nchini Misri, vyombo vya habari vilipeperusha habari hiyo kwa utofauti mkubwa.
Peter Greste ,ndiye alikuwa anaripoti matukio nchini Misri Disemba mwaka jana wakati wa harakati za mapinduzi.
Kisha yeye na wenzake wawili wakatuhumiwa kwa kusaidia vuguvugu la kigaidi na kutangaza taarifa za kupotosha dhidi ya serikali na maslahi ya taifa hilo.
Madai ambayo serikali ya Australia imekuwa ikikanusha vikali.
Serikali ya Australia ilitoa taarifa yake
ikisema kuwa imeshtushwa sana na uamuzi wa mahakama katika kesi ya Peter
Greste. Imeelezea kushangazwa sana na hukumu iliyotolewa. Serikali
imesema haielewi kabisa matukio haya.
Chanzo bbcswahili
BONYEZA HAPA
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment