Serengeti:Ni
jambo la kawaida kuwaona wanaume wilayani Serengeti wakiongozana na
wake ama watoto wao siku za minada, kwenda kuuza mifugo ili wanunue
mahitaji yao, lakini mapato hudhibitiwa na wanaume.
Mara
baada ya mauzo na kununua mahitaji,wanawake na watoto hulazimika kurudi
nyumbani huku wanaume wakibaki wakistarehe ,huzitumia siku ,ni nadra
mwanaume kuwahi kurudi nyumbani .
Mei 19,
Rhoda Nyangi Mtatiro (24) mkazi wa Kitongoji cha Kenyana kijiji cha
Masangura kata ya Ring’wani wilayani Serengeti, licha ya ujauzito wa
miezi sita alionao alikubali kuongozana na mumewe Wang’enyi Sabai(30)
kutoka kijijini kwao hadi Rung’abure umbali wa kilometa zaidi ya 15 kwa
mguu.
Huku
wakiswaga kondoo wanne walifanikiwa kufika mnadani na kuwauza
wakajipatia fedha za mahitaji hakujua kuwa kuna balaa lingemkuta siku
hiyo, pamoja na kuswaga na kutembea umbali mrefu na ujauzito wake
hakuambulia kitu zaidi ya kipigo ambacho leo hajui hatima ya maisha
yake.
Licha ya
kufanikiwa kuuza kondoo wote aliambulia Sh 2,000 kwa ajili ya kununua
nguo za mtoto wao mmoja kati ya wanne walionao anayesoma darasa la
kwanza shule ya Msingi Geitasamo, iliyoko hapo Rung’abure ambako ni kwao
na Rhoda.Ilikuwaje?
“Nilizunguka
kutafuta nguo za mtoto, wakati huo mume wangu alikuwa nyumbani kwetu
anamsalimia mama mkwe…. Saa 11:30 jioni nilifika nyumbani na kuwaambiwa
ameishaondoka kurudi kijijini kwetu….nilishindwa kuondoka pekee yangu
kwa muda huo na hali niliyonayo nikalala kwetu, ikawa mwanzo wa
matatizo,”anasema.
Anasema
alilazimika kutoka saa 12 alfajiri na kufika kwake saa tano asubuhi
akiwa amechoka ,na kwenda kumsalimia mume wake dukani, hata hivyo
alivyopokewa akahisi atapata adhabu kwa kuwa mume wake hana namna
nyingine ya kuwasilisha hisia zake zaidi ya kutembeza kipigo, akaamua
kuaga na kurejea nyumbani.
“Nilishangaa
kuona mume wangu akifunga duka huku akiwa ameshikilia panga na kamba
ananifuata …mita kadhaa akanifikia na kuniamru nisimame, eneo lenyewe
limejaa vichaka….niliingiwa na hofu, ghafla akauliza nilikolala…kwa
kujiamini nikamwambia nililala nyumbani kwetu baada ya kuogopa kutembea
pekee yangu jioni,” anasema na kuongeza:
“Akasema
ameambiwa nilikuwa na mwanaume gesti….nilimtaka anielewe kuwa nililala
kwetu baada ya kuniacha…na ujauzito huo ninawezaje kwenda na mwanaume
gesti….ikawa kama amechokozwa maana aliniamuru ninyanyue mikono juu na
kuanza kunishambulia kwa mateke tumboni, kama vile haitoshi akaanza
kunikata miguu kwa panga ili niseme kuwa nilikuwa na mwanaume gesti,”
anasema kwa masikitiko.
Afungwa kwenye kiti
Pamoja na
maumivu ya kupigwa tumboni na kukatwa miguu, alifungwa kwenye kiti na
kuendelea kuadhibiwa mbele ya mama mkwe wake Rhobi Sabai na mke Mwenzake
Rhobi Kibina(20), hadi akapoteza fahamu, hata hivyo alijikuta
amefungiwa ndani ya nyumba na kuambiwa kuwa aliokolewa na jilani yao
Moya Marwa.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment