Mshambuliaji
wa Timu ya Taifa ya Uruguay ,Luis Suarez ameibua mgogoro mkubwa huko Brazil
baada kuonekana akimuuma Meno Beki wa Italia Giorgio Chiellini kwenye Mechi ya
mwisho ya Kundi D la Fainali za Kombe la Dunia ambayo Uruguay waliitoa Italia
kwa bao 1-0 (June 24, 2014) na wao kutinga Raundi ya Pili ya 16 bora.
Tukio hilo
lilitokea Dakika chache kabla ya Bao la Kichwa la Dakika ya 81 la Diego Godin
kuwapa ushindi Uruguay.

Mara baada
ya tukio hilo la kung’atwa, Chiellini aliinua Jezi yake kumwonyesha Refa Marco Rodriguez wa Mexico ambae hakuchukua
hatua yeyote.
Aprili 2013,
Luis Suarez alifungiwa Mechi 10 kwa kumuuma Meno Beki wa Chelsea Branislav
Ivanovic kwenye Mechi ya Ligi Kuu Uingereza.
Mwaka 2010
huko Uholanzi, Suarez alifungiwa Mechi 7 kwa kumuuma Kiungo wa PSV Eindhoven
Otman Bakkal.
Giorgio akimuonyesha sehemu alipong'atwa meno na mshambuliaji wa Uruguay Luis Suarez refa kitendo hicho akukiona
Miaka minne
iliyopita huko Afrika Kusini kwenye Fainali za Kombe la Dunia Suarez alizuia
Mpira uliokuwa ukitinga Golini kwenye Dakika ya 120 kwa Mkono wake na yeye
kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu, Ghana kupewa Penati ambayo Asamoah Gyan
aliikosa na hatimae Uruguay kutinga Nusu Fainali kwa Mikwaju ya Penati.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro








Post a Comment
Post a Comment