Muda
mchache baada ya timu yake kuondolewa rasmi kwenye michuano ya kombe la
dunia kwa kushindwa kufanya vyema katika mechi za makundi kwa mara ya
pili mfululizo katika kombe la dunia, kocha Cesar Prandelli amefanya
maamuzi magumu.Italia iliondolewa baada ya kufungwa kwa goli 1-0 na
Uruguay katika mechi ya mwisho ya makundi.Baada ya mchezo Prandelli
akiwa kwenye mkutano wa waandishi wa habari alitangaza kujiuzulu
kuifundisha timu hiyo.“Nilichagua mfumo fulani wa ukufunzi na ndio
sababu ninajiuzulu, kwa sababu haukufanya kazi,” alisema.
Aliongezea:
“Kuna jambo ambalo limebadilika tangu nilipotia saini mkataba mpya.
Sijui kwanini lakini sina haja ya kutafuta sababu .”
Kocha
huyo aliingia mkataba mpya na Italy Mei mwaka huu ambao ungemfanya
aendelee kuifundisha Italy hadi baada ya mashindano ya kuwania ubingwa
wa Euro ya mwaka wa 2016.
Prandeli amechukua hatua hii baada ya kujiuzulu kwaa rais wa shirikisho la kandanda la Italia Giancarlo Abete.
“Nilizungumza
na rais wa shirikisho na naibu wa rais Demetrio Albertini na nikawapa
barua ya kujiuzulu kwangu. Ni jambo lisilobadilika,”
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro








Post a Comment
Post a Comment