
Nyota: Lionel Messi (juu) aliifungia mabao mawili Argentina dhidi ya Nigeria.
TIMU
ya Taifa ya Nigeria maarufu kama Super Eagles imefanikiwa kufuzu hatua
ya 16 ya kombe la dunia licha ya kufungwa mabao 3-2 dhidi ya Argentina.
Mshambuliaji
hatari wa kikosi cha Alejandro Sabella, Lionel Messi amefunga mabao
mawili katika dakika ya 3 na 45 katika ushindi uliowapa Argentina
ushindi wa asilimia 100 katika kundi lao la F.
Bao la tatu la Argentina limefungwa na Marcos Rojo katika dakika ya 50.
Mabao mawili ya Nigeria yamefungwa na Ahmed Musa katika dakika ya 4 na 47.
Katika michuano ya mwaka huu, dhahiri, Argentina inamtegemea zaidi Messi katika mechi zake.
Baada ya kufunga mabao hayo, kocha Sabella alimpumzisha nyota huyu wa FC Barcelona kwa ajili ya mikikimikiki ya hatua ya 16.
Pia
Sabella alishuhudia mshambuliaji wake, Sergio Kun Aguero akitolewa nje
ya uwanja kwa kile kilichoonekana kupata maumivu ya misuli tena.

Asante mungu: Messi akinyosha vidole kama ishara ya kumshukuru mungu baada ya kufunga .
BOSNIA 3 vs 1 IRAN


Mshambuliaji wa Manchester City akifunga bao lake la kuongoza.

Kipa wa Iran Alireza Haghighi aliambulia manyoya tu.
kama huja jiunga nasi kwenye ukurasa wetu wa facebook kwa habari zaidi BONYEZA HAPA
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment