Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
 Msanii wa vichekesho kutoka Kundi la Vituko Show, Ismail Makombe ‘Mapembe’.
MSANII wa vichekesho kutoka Kundi la Vituko Show, Ismail Makombe ‘Mapembe’, anadai kuingizwa mjini na staa mwenzake, Mussa Yusuf Kitale ‘Mkude Simba’ kwa kumuahidi kumchangishia pesa na mwisho kuingia mitini.

Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni, Mapembe ambaye hali yake ni mbaya kiafya alisema:
 
“Ndugu yangu kweli hujafa hujaumbika, naumwa kweli nakosa msaada wa karibu kutoka kwa wasanii wenzangu na leo naishia kutoa lawama huku wengine wakiniingiza mjini kama alivyonifanyia Kitale aliyeniahidi kunichangishia pesa na kunikataza kuombaomba kwa madai ya kuitia aibu tasnia yetu lakini mpaka leo.”
Staa wa Maigizo upande wa vichekesho, Mussa Yusuf Kitale ‘Mkude Simba’.
Baada ya kupata madai hayo, paparazi wetu alimtafuta Mkude Simba ‘Kitale’ na alipopatikana alisema: 

“Ni kweli Mapembe nilimuahidi kumchangishia pesa ila baada ya wazo hilo kulifikisha kwenye chama chetu cha komedi viongozi waligoma kumsaidia kwa madai kuwa yeye siyo mwanachama wao na hata kipindi chama kinaanzishwa aligoma kujiunga kwa kuona hakina maana hivyo nao wamekataa, kwa hiyo hana sababu ya kunilalamikia.”

BONYEZA HAPA 

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top