Mwimbaji wa kike wa Nigeria mwenye umri wa miaka 23 anaefahamika kwa
jina la Adokiye ameeleza anachofikiria kuhusu wasichana zaidi ya 200
wanaoshikiliwa na kundi la Boko Haram.
Mwimbaji huyo ambaye anafahamika sana kwa comments zinazotengeneza mijadala hudai kuwa yeye ni bikira.
Mwishoni mwa wiki hii ameiambia Showtime kuwa anajitoa yeye kwa kundi
la Boko Haram kama inawezekana wao kuwaachia wasichana wanaoshikiliwa na
kundi hilo.
“Sasa hivi ni saa tato usiku, je unajua ninachofikiria? Wale
wasichana wadogo, wapi walipo na nini kinawatokea muda huu. Sio sawa. Ni
wadogo sana.
"Nawishi ningeweza kujitoa mimi kubadilishana nao. Wana
umri kati ya miaka 12 hadi 15. Mimi ni mkubwa na nimeshazoea maisha
zaidi yao.
"Hata kama wanaume 10 hadi kumi na mbili watanichukua kwa
usiku mmoja, sijali. Nachojali wawaachie hao wasichana warudi kwa wazazi
wao.”
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment