
Mwanamke wa Sudan aliyehukumiwa kifo kwa madai ya kuasi dini ya kiislam ameachiliwa huru baada ya kushikiliwa kwa mara ya pili.
Meriam
Ibrahimu alikwenda katika ubalozi wa Marekani uliyopo mji Mkuu wa
Khartoum.Mumewe ana asili ya Sudan Kusini lakini kwa sasa ni raia wa
Marekani.Mwanamke huyo aliachiliwa baada ya kuhukumiwa adhabu ya kifo
siku ya jumatatu lakini alishikiliwa tena na polisi kwa tuhuma za
kughudhi hati za kusafiria ili aondoke nchini Sudan kwenda Marekani.
Kufuatia kuachiliwa huru kwa mara nyingine, Mke huyo wa Ibrahim ameiambia BBC kwamba ataendelea kuwa Mkristo.
Kesi yake ya kuasi dini imevuta hisia za watu wengi wakiwemo watetezi wa haki za binadamu pamoja na nchi za Magharibi.
BBC
kama huja like ukurasa wetu wa facebook kwa habari zaidi BONYEZA HAPA
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment