Asia Hakika anayedai kuharibiwa mali zake na dereva taksi aitwaye Lindoya.
Mlalamikaji Asia, mkazi wa Tabata – Chama na mtuhumiwa Lindoya mwenye makazi yake Mbezi – Makabe ni wapenzi wa muda mrefu sasa, lakini baada ya Asia kugundua kuwa mwenzake ana mke na watoto, akagoma kumpa tendo la ndoa, jambo lililoibua kisanga hicho.
Akizungumza na Uwazi, Asia alisema: “Lindoya ni mpenzi wangu, tulikuwa tunaelekea kuwa mume na mke, maana tumeishi kwa miaka miwili sasa, lakini siku zote amenieleza kuwa hana mke wala watoto, lakini nimegundua kuwa alinidanganya.
Asia Hakika akiangalia mali zake zilizoharibiwa.
“Ana mke na watoto wawili, nikaamua nimuache aendelee na familia yake.
Akakataa,
anataka kunitumia tu. Nilipomkatalia ndiyo akaamua kuniharibia vitu
vyangu. Alinikuta nina vitu vya ndani nilivyonunua kwa fedha zangu,
nimepanga chumba kwa pesa yangu na aliniomba tuishi pamoja
nikamkubalia.
“Baadaye akaanza kujenga nyumba huko Mbezi ya Makabe, nilifurahi sana niliamini kuwa tukioana tutakua tunaishi huko lakini cha kushangaza baada ya kumaliza kujenga alimfuata mkewe huko Mbeya, wakahamia na watoto wake.”
Alisema, mpenzi wake huyo zilipendwa, alimwambia asikanyage nyumbani kwake kwa kuwa mkewe amekuja, jambo ambalo alikubaliana nalo kwa sharti kuwa wasitishe uhusiano wao lakini Lindoya akaonekana kutoridhika.
Baadhi ya mali za Asia Hakika zilizoharibiwa.
“Siku moja nikiwa kazini, alifika nyumbani kwangu akafungua mlango kwa funguo wake, maana kila mmoja alikuwa na wake; akaharibu mali zote ndani, akaacha kitanda tu. Nimeumia sana kwa kweli,” alisema Asia.
Kwa sasa kesi hiyo ipo katika Kituo cha Polisi Tabata kwa uchunguzi ambapo jalada la uchunguzi limeandikishwa kwa namba TBT/IR/2032/2014.
>>>GPL
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment