Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Jambazi aliyetoka jela kwa msamaha wa rais afanya tena mauaji kwa kunyonga!Pichani: Mazishi ya dada aliyenyongwa

Mtu mmoja anayedhaniwa kuwa ni jambazi anatafutwa na jeshi la polisi kwa madai ya kufanya matukio mbalimbali ya kiharifu likiwemo tukio la hivi karibu kumnyonga hadi kufa dada mmoja aliyetajwa kwa jina la Bahati Husein mkazi wa Ulongoni A Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam.


Akizungunza na 100.5 times fm, dada wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Moshi Hussein alisema mtu huyo ambaye anatambulika kwa jina moja la Godfrey, kabla ya kumuua dada yake alikuwa akimtamkia mara kwa mara kwamba ipo siku atamuua.


“Tulikuwa tunaona kama utani maana alikuwa akisema suala la kumuua mara kwa mara na siku chache kabla ya kumuua walikuwa na ugomvi ambapo Godfrey alikuwa akimhisi dada yangu (ambaye kwa sasa ni marehemu) anamahusiana na mwanaume mwingine hali iliyosababisha kaka aje na kuwasuruhisha,” anaeleza Moshi huku akilia kwa uchungu.


Aliendelea kusema baada ya kusuruhishwa alionekana kuridhika na kumtaka mkewe (marehemu) ampikie ugali ambapo marehemu alifanya kama alivyoagizwa lakini usiku wake akambyonga hadi kufa.


“Baada ya kumuua aliondoka usiku huo huo na asubuhi alipiga simu kwa ndugu akisema eti anataka kuongea na mkewe kwa hiyo mtu aende ampe simu ili wazungumze wakati anajua nini amekifanya!” anasimulia Moshi.


Alipoulizwa wao walijuaje kama marehemu alinyongwa hadi kufa, Moshi alisema baada ya kifo hicho walikwenda kuripoti kituo cha polisi Stakishali ambapo kabla ya kujua kama ndugu yao ni marehemu walimchukuwa na kumkimbiza katika Hospitali ya Amana ambapo mara baada ya madaktari kumchukuwa vipimo iligundulika kuwa dada tayari alikuwa mfu. Bonyeza hapa kuendelea kusoma

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top