Wasomi wanapokutana hasa katika zoezi
la kutunukiwa cheti kama kielezo cha uhitimu wa ngazi fulani kuna vitu
huwezi kuvifikiria kama vitatokea hata kidogo.
Katika Jack Britt High School, North
Carolina, Marekani wanafunzi mmoja amewaacha hoi mamia ya watu
waliohudhuria sherehe ya kutunukiwa vyeti (graduation) baada ya kupanda
jukwaani kupokea cheti chake na ghafla akavua johon lake na kubaki na
boxer.
Baada ya kuvua joho alinyoosha mikono yote
miwili juu kama mwanamieleka anayetamba. Lakini haikuchukua round
wanausalama wakamdhibiti na kumuweka chini ya ulinzi.
Kwa mujibu wa The Huffington Post, kijana huyo alinyang’anywa diploma yake na hivyo hakukabithiwa cheti.
Hata hivyo bado anahesabiwa kama mtu aliye maliza masomo yake na kuhitimu licha ya kuwa hana kielelezo cha elimu yake.
“Shule yetu imefanya jitihada kubwa. Hapo
zamani watu waliohudhuria walikuwa wenye vurugu wakati wa graduation.
Tumefanya jitihanda kuwafanya watu waheshimu wanafunzi. Huyu kijana
amechagua kutoonesha heshima kwa wanafunzi wenzake.” Alisema Dr Frank
Till, mwalimu wa chuo hicho.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment