Wakati rafiki yake kipenzi, Wema Sepetu akidaiwa kunasa mimba ya
Diamond , Aunt Ezekiel yeye amesema bado hajaona mwanaume
anayeweza kumtia mimba na hatimaye kuitwa baba wa watoto wake.
Akipiga stori na mwanahabari wetu , Aunt Ezekiel amedai kuwa
kuna wakati unaweza kumuona yupo kwenye ndoa au uchumba lakini
haimaanishi kuwa kuwepo katika mazingira hayo ndo anaweza
kuzaa au kushika mimba kwani suala hilo kwake ni kubwa sana
na hajafikiria kama linaweza kutokea kwa sasa…
“Siyo kwamba sina uwezo wa kubeba mimba, hapana, suala kubwa hapa ni kwamba bado sijaona mwanaume wa kunizalisha.
“Ni kweli nilikuwa kwenye ndoa lakini sikutaka kubeba mimba na
ndo maana hadi sasa hivi nipo kama ninavyoonekana,” alisema
Aunt Ezekiel
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment