Wanamgambo wa Al-shabaab nchini Somalia wamewakamata
takriban wanawake mia moja na kuwaaamuru kuvalia mavazi yanayostahili kwa
wanawake wa kiislamu kuambatana na sheria za dini hiyo la sivyo wapate kichapo.
Wanawake hao walikamatwa sokoni katika eneo la Buala karibia
kilomita mia tatu Kusini-Magharibi mwa Mogadishu.Mwandishi wa BBC nchini humo
Mohamed Mohamed anasema ni nadra kwa Al-shabaab kuwakamata watu wengi kwa
wakati mmoja kama hivyo.
Baadhi ya wanawake hujifunika gubigubi kutoka kichwani hadi
miguuni
Mwandishi wa BBC anasema kuwa wanawake hao walivalia mavazi
mapesi na kukosa kujifunika nyuso zao kutokana na joto kali
Wanawake hao waliamrishwa kuvaa Niqab,vazi linalowafunika
mwili mzima huku sehemu ndogo ya uso ikiachwa nje ili kuwawezesha kuona.Jina al
shabaab linalo maanisha "vijana" kwa kiarabu,linapigania mfumo wa
kiislamu wa wahhabi saudia.Watu ambao washawahi kupatikana na kosa la Zinaa
wamepigwa mawe hadi kufa na wezi kukatwa mikono.
Serikali ya Somalia inayofadhiliwa na umoja wa
mataifa,ikisaidiwa na wanajeshi wa Muungano wa Afrika, imefaulu kutimua
Al-shabaab nje ya miji mikubwa nchini humo lakini kundi hilo bado linaendelea
kutekeleza mashambulizi huko.
BBC
BONYEZA HAPA
BONYEZA HAPA
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment