Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

http://kiswahili.irib.ir/media/k2/items/cache/bdef8f4cae614fb5e663075ff4dbe019_L.jpg
Waziri wa Usalama wa Taifa wa Somalia amejiuzulu. Abdikarim Hussein Guled amejiuzulu baada ya kujiri shambulio la kigaidi karibu na bunge la Somalia mjini Mogadishu hapo jana. Taarifa zinasema kuwa, baada ya shambulio hilo lililopelekea watu 10 kuuawa, waziri huyo wa usalama wa Somalia alishinikizwa na wabungen ajiuzulu.

 Wakati huo huo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelaani shambulio hilo lililofanywa na wanamgambo wa al Shabab kwenye jengo la bunge la Somalia. Wajumbe wa Baraza la Usalama wamesema kuwa wanasikitishwa na shambulio hilo dhidi ya bunge taasisi ambayo inawakilisha wananchi wa Somalia, na ambako ni mahala wanapotumaini kupata usalama, amani na maendeleo kwa njia  halali.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top