Bwana Gasto Edward na mkewe ambaye anadaiwa kumkata nyeti zake.
Gasto Edward (32) amemkata mkewe Mwelu Raymond sehemu zake za siri, Risasi Jumamosi lina simulizi hii ya kusikitisha. Tukio hilo lilitanguliwa na kumpiga mkewe huyo na kipande cha nondo kichwani hali iliyosababisha apoteze fahamu papo hapo na kutekeleza azma yake.Imeelezwa kuwa, tukio hilo lenye sura ya majonzi, lililovuta hisia za watu wengi lilitokea Jumatano ya wiki hii, huko King’azi, Kwembe – Mbezi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
KISA CHA YOTE
Habari
zilizopatikana eneo la tukio zinadai kuwa, chanzo cha unyama huo ni
wivu wa kimapenzi ulioingilia ndoa hiyo, ambapo Gasto alimtuhumu mkewe
kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanaume mwingine anayeishi Temeke
aliyejulikana kwa jina la Mgogo.
Chanzo
chetu cha kuaminika, kwa sharti la kutotajwa gazetini kilisema: “Mwelu
na Gasto wametoka mbali, wameishi kwa muda mrefu na wamebarikiwa watoto
wawili, sema siku za hivi karibuni, Gasto alianza kumtuhumu mkewe kuwa
anatoka nje ya ndoa.
“Tena
siyo tuhuma, anasema alikuwa akimwambia wazi kuwa ana mwanaume wake
Mgogo ambaye yupo Temeke. Jamaa alikuwa analalamika kuwa mkewe alifikia
hatua ya kumwambia amuache ili aende kwa mwanaume huyo anayejua
kutunza.”
Akaongeza:
“Unajua katika hali ya kawaida, kama ni kweli mke alikuwa akimwambia
mumewe maneno ya hovyo kama hayo, yanaumiza. Ndiyo maana jamaa akaona
kwa sababu chanzo cha yote ni penzi, akamkata nyeti zake.”
MJUMBE ANAFAFANUA
Mjumbe
wa Mtaa wa King’azi, Amani Abdallah alikiri kupokea malalamiko hayo
kutoka kwa Gasto, mwezi mmoja uliopita na kufanikiwa kusuluhisha.
“Ni
kweli walikuwa na tofauti na hili suala lilinifikia hata mimi. Gasto
alikuja kulalamika kuwa mkewe siyo mtulivu na anamwonyesha dharau.
Lakini tulisuluhisha yakaisha. Jana (Jumatano) ambapo tukio lilitokea,
yule mkewe alikuja kulalamika kuwa mumewe amebadilika.
“Alisema
amemuona akinoa kisu asubuhi, usiku ugomvi ukatokea akaamua kuja kulala
kwangu, lakini baadaye akaniaga anakwenda kulala kwa jirani yao mama
Mbonde, huko ndipo mumewe alipokwenda kumchukua na kumfanyia unyama
huo.”
WOSIA MZITO
Baada
ya tukio hilo, Gasto alitoroka lakini aliandika wosia uliomtaja mrithi
wa mali zake kuwa ni watoto wake Edward na Editha ambapo alimchagua
kabisa msimamizi wao kuwa ni mdogo wake aitwaye Kiriani.
Jalada alilofunguliwa Gasto.
Katika
barua hiyo, Gasto alisema anakwenda kujiua kwa sababu amechoshwa na
dharau za mkewe, ndiyo maana akaamua kuondoa sehemu zinazompa kiburi.
Kesi ya Gasto imeripotiwa katika Kituo cha Polisi Kwa Yusuph na kufunguliwa jalada nambari KWR/RB/4716/14 – KUJERUHI.
Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Camilius Wambura alipopigiwa
na Risasi Jumamosi ili kuelezea tukio hilo, alikiri kupokea taarifa,
akasema bado wanafuatilia.
Credit:GPL
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment