Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

UKATILI: MTOTO MLEMAVU AFUNGIWA NDANI NA MAMA YAKE KWA MIAKA 9 KOROGWE TANGA

Mtoto mwenye ulemavu wa akili wilayani Korogwe, mwenye umri wa miaka 15, amefungiwa chumbani na mama yake wa kambo kwa muda wa miaka 9, ambapo amekuwa akijisaidia humo choo kikubwa na kidogo, kisha kuwekewa chakula katika bakuli lake maalum ndani ya chumba hichoMwandishi wetu ameshuhudia mtoto huyo akiwa chumbani na upande mmoja wa kanga huku kukiwa na vinyesi na bakuli lake analowekewa chakula mithili ya mnyama
.

Mama mlezi wa mtoto huyo mlemavu aliyejulikana kwa jina la Khadija Makame alipoulizwa kuhusu kitendo cha kumfungia ndani mtoto huyo, amesema kuwa huwa anamtoa nje kwa chakula na hata kumsindikiza chooni, majibu ambayo majirani walipingana naye baada ya kushuhudia ndani ya chumba chake kukiwa na vinyesi na bakuli lake la kulia.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top