MWANAFUNZI wa Shule ya Msingi Liami wilayani Ifakara mkoani Morogoro (jina limehifadhiwa), amebakwa na watu wasiojulikana alfajiri ya Mei 5, mwaka huu nyumbani kwa bibi yake.
Akizungumza
mama wa binti huyo mwenye umri wa miaka 13, Neema Ally akiwa wodi A ya
watoto katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alisema mtoto wao alienda
nyumbani kwa bibi yake kulala baada ya kumaliza kula kwa wazazi wake.
Alisema
watu waliofanya unyama huo, pia waliiba baiskeli kabla ya mtoto wao
kuokolewa na wasamaria wema waliosikia mayowe yake ya kuomba msaada
ambapo walimkuta akitokwa na povu mdomoni.
Alisema wasamaria wema hao walimkuta mtoto wake akiwa amepoteza fahamu kutokana na kukabwa koo wakati akifanyiwa kitendo hicho.
alisema Neema.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, ACP Leonard Paul amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro








Post a Comment
Post a Comment