Kama Diamond Platnumz
angekutana na Eiden usiku wa kuamkia Jumamosi ya leo, huenda angemfanya
mwanamke huyo wa kizungu kuwa mwenye furaha kuliko watu wote duniani. Mwanamke
huyo ambaye usiku huo alikuwa akisherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa kutimiza
miaka 32, anadai alisafiri kutoka nchini Rwanda kuja jijini Dar es Salaam ili
amtafute hitmaker huyo wa ‘Number One’ amuimbie wimbo maalum wa siku ya
kuzaliwa.
Bahati mbaya, mara tu
baada ya kutumbuiza kwenye show ya Road to MAMA, aliwahi ndege ya kwenda jijini
London, Uingereza kuwahi show yake na Ommy Dimpoz na kuizima ndoto ya Eiden.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro








Post a Comment
Post a Comment