*************
Mtu mmoja amenusurika kufa baada ya kulipukiwa
na bomu lili lotengenezwa kienyeji kisha
kuhifadhiwa katika mfumo wa zawadi na kutegwa
katika nyumba ya kupumzikia wageni iliyopo
kanisani la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT jijini
Mwanza usiku wa kuamkia leo.
Majeruhi huyo ambaye ni mhudumu wa nyumba
hiyo Benadeta Alfred amelazwa katika hospitali ya
Rufaa Bugando ambapo anapatiwa matibabu
baada ya kujeruhiwa vibaya sehemu kubwa ya
mwili wake
Kutokea kwa mlipuko huu wa bomu katika eneo
hili la kanisa kunaacha maswali mengi kwa wakazi
wa jiji la Mwanza na waumini wa kanisa hili
Bomu hili lilowekwa kwa mfumo wa zawadi ndani
ya nyumba ya kupumzikia linadaiwa kuwa hapa
kwa mda wa siku tatu bila kufahamu mwenye
mzigo huu na kilichomo ndani yake
Licha ya uimara wa fensi na ulinzi uliopo katika
eneo hili la kanisa maswali mengi yanaibuka juu
ya mhusika aliyeingiza bomu hilo na kwa njia
gani.
Kikosi maalum cha uchunguzi wa milipuko
kimewasili kutoka jijini Dar es salaam kufanya
uchunguzi katika eneo hili la mlipuko.
Aidha wito umetolewa kw awananchi wote kuwa
makini na vitu wasivyovijua ili kujiepusha na
madhara kama haya.
Juhudi za kunusuru maisha ya Benardeta
zinaendelea hapa katika hosptali ya rufaa ya
Bugando katika chumba cha ungalizi maalumu.
Matukio ya milipuko inayosadikiwa kuwa mabomu
imeendelea kurindima nchini hasa katika mikoa ya
Arusha, visiwani Zanzibar na sasa jijini Mwanza,
hali ambayo inaacha swali kwa jeshi la polisi juu
ya usalama wa raia katika maeneo yasio rasmi na
ya umma.

ya umma.Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro

Post a Comment
Post a Comment