Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
TIMU
ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars imefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao
1-0 dhidi ya Malawi katika mchezo wa kimataifa wa Kirafiki uliopigwa
jioni ya leo Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Bao
pekee la Stars limefungwa na kiungo mahiri, Amri Ramadhan Kiemba katika
dakika ya 35 akimalizia kazi nzuri ya Shomary Kapombe.
Leo
hii kocha wa timu wa Taifa Stars, Mholanzi Mart Nooij hakuanzisha
kikosi chake kinachojulikana kuwa cha kwanza kwa lengo la kujaribu
wachezaji wanaoweza kumsaidia katika mchezo wa marudiano dhidi ya
Zimbabwe mjini Harare.
Kama
ilivyokawaida, Nooij alimuanzisha mlinda mlango Deogratius Munish
`Dida`, Himid Mao, Edward Charles, Said Mourad, Joram Mgezeke, Shomary
Kapombe, Simon Msuva, Erasto Nyoni, Kevin Friday, Amri Kiemba na Khamis
Mcha `Vialli`.
Katika
kipindi hicho, Stars haikucheza vizuri sana tofauti na wapinzani wao
Malawi ambao unaweza kusema walikosa bahati ya kufunga.
Kipindi
cha pili, Nooij alibadilisha karibu kikosi chote ambapo wachezaji kama
Kevin Yondan, Ramadhan Singano, Frank Domayo, Said Juma, Mwinyi
Kazimoto.
Ushindi
wa leo unatoa taswira nzuri kwa Stars kuelekea Harare ambapo wanaenda
wakiwa na kumbukumbu nzuri ya ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa kwanza
uliopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam
Stars
wanaotarajia kuondoka ijumaa mei 30 mwaka huu kwa mujibu wa taarifa
kutoka TFF, wanahitaji ushindi sare ya aina yoyote au ushindi ili kwenda
sehemu inayofuata.
Aidha Afisa habari wa shirikisho la soka Tanzania Boniface Wambura Mgoyo amesema wameandikia TP Mazembe wakiomba kuwapata wachezaji wawili wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu na kabla ya ijumaa wanatarajia kupata majibu.
Aidha Afisa habari wa shirikisho la soka Tanzania Boniface Wambura Mgoyo amesema wameandikia TP Mazembe wakiomba kuwapata wachezaji wawili wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu na kabla ya ijumaa wanatarajia kupata majibu.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment