Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
SIRI nzito yaanikwa juu ya utata wa nani mrithi wa gari alilokuwa akitumia marehemu Maalimu Mhidini Gurumo huku pia gazeti hili likibaini kuwa kadi ya gari hilo ipo kwa Ruge Mutahaba.

Diamond Platinum akimkabidhi ufunguo ya gari aina ya Toyota Fun Cargo marehemu Gurumo.
Ruge ni Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Kampuni ya Clouds Media Group ya jijini Dar es Salaam.
Mbali na kujulikana kuwa kadi hiyo ipo mikononi mwa Ruge, gazeti hili lilichimba na kugundua mmiliki halali wa gari hilo aliyeteuliwa na marehemu Gurumo kabla mauti kumkuta.
SIKIA CHANZO

Kwa sharti la kutotajwa jina lake gazetini, chanzo chetu kilisema: “Mgogoro uliopo kati ya watoto wa marehemu ni kazi bure tu. Lile gari ameachiwa mke wa marehemu, huo ndiyo ukweli wa mambo.”

Akaongeza: “Ndiyo maana hata marehemu alimwagiza Diamond (Nasibu Abdul) ampatie Ruge kadi ya gari ili abadilishe jina liwe na mkewe. Watoto wanazozana bure tu.”
DIAMOND NAYE

“Ni kweli kabisa, mzee (marehemu Gurumo) aliniagiza nimpe kadi Ruge ili ashughulikie ubadilishwaji wa jina, ndivyo nilivyofanya. Mpaka sasa bado Ruge anaendelea kushughulikia.”
Diamond hakufafanua zaidi, hata pale alipoulizwa maswali mengine, alisema atafutwe Ruge kwa maelezo kuwa anaweza kutoa ufafanuzi mzuri zaidi.
Gari aina ya Toyota Fun Cargo alilopewa mzee Gurumo na Diamond.
RUGE SASA
Ruge alipopatikana kwa njia ya simu hakuuma maneno, aliweka wazi kuwa ni kweli kadi ipo kwake na kwamba alipewa na Diamond ikiwa ni maagizo ya marehemu Gurumo ibadilishwe jina, liwe na mkewe.

“Ujue marehemu Gurumo kabla hajatutoka alishtukia kuwepo na mgogoro juu ya gari hilo kwa wanaye hivyo akamuomba Diamond kwa kipindi hicho asimpatie kadi ya gari mpaka itakapobadilishwa na kuwa na jina la mkewe,” alisema Ruge na kuongeza:
“Baada ya marehemu kuulizwa sababu ya kuchukua uamuzi huo alisema kuwa anayestahili kuwa mmiliki wa gari hilo ni mkewe kwani aliyempatia gari alikuwa na lengo la kumsaidia yeye na si watoto wake...sasa gari lingeandikwa jina lake lingeleta utata zaidi wa haya yanayoanza kujitokeza sasa.”
Mzee Gurumo enzi za uhai wake.
Ruge anaendelea kufafanua: “Marehemu alisema watoto bado wana nguvu tofauti na mkewe ambaye tayari ameshazeeka hivyo ni vyema likitumika kumsaidia, kwa hiyo mrithi halali wa hilo gari kwa mujibu wa marehemu mwenyewe ni mkewe na si vinginevyo.” 
>>>>>GPL
   <<<<<BOFYA HAPA ULIKE PAGE YETU>>>>>  
 

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top