(Picha ni majambazi waliokamatwa kuhusiana na tukio hilo).
Jeshi
la Polisi Wilayani Mpanda Mkoa wa Katavi linawashikilia watu watatu kwa
tuhuma za kumuuwa Bodaboda mmoja aitwaye Frenk Joseph (25)mkazi wa mtaa
wa Nsemlwa Wilayani Mpanda Mkoa wa Katavi kwa kumchinjashigo na kisha
kumpola pikipiki yake aina ya SANLG yenye namba za usajiri T 704 CDQ
Kamanda wa jeshi la Polisi wa Mkoa wa Katavi
Kamishina msaidizi mwandamizi
Dhahiri Kidavashari aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Charles
Kidaha(29),Madia Mtema (40) na Buyenza Jendesha (40) wote wakazi
waTarafa ya Mwese Wilayani Mpanda.
Kidavashari alisema watuhumiwa
hao walimuuwa bodaboda huyo hapo Aprili 26 mwaka huu majira ya saa saa
kumi na moja jioni huko katika eneo la Kijiji cha Mpembe Tarafa ya Mwese
Wilayani Mpanda.
Siku hiyo ya tukio marehemu
Samwel alikuwa kwenye kijiwe chake cha Bodaboda kilichoko kwenye
hospitali ya Wilaya ya Mpanda akiwa na pikipiki yake aina ya Sunlg yenye
Namba za usajiri T704CDQ aAlisema wakati akiwa kwenye kituo hicho cha
Bodaboda alitokea mtu asiye fahamika na kumkodisha marehemu ambapo
waliondoka nae huku marehemu akiwa aja waaga bodaboda na kuwafahamisha
mahari alikokuwa wakielekea na mteja wake huyo.
Alifafanua kuwa ndipo siku
iliyofuata ya tarehe 27 Aprili mwili wa marehemu bodaboda huyo
ulipoonekana ukiwa umetelekezwa porini katika kijiji cha Mpembe huku
akiwa amechinjwa na kitu chenye ncha kali na pikipiki yake haikuonekana
katika eneo hilo.
Kamanda Kidavashari alieleza
kuwa baada ya tukiola mauwaji hayo polisi waliendelea kufutilia tukio
hilokwa kushirikiana na raia wema na ndipo hapo mei 22 majira ya saa
kumi na moja jioni huko katika kijiji cha Kasekese Kata ya Simbwesa
Wilaya ya Mpanda raia wemawalitowa taarifa kwa jeshi la polisi kuwa
wanamashaka na watuhumiwa hao kwani waliwasili kijijni hapo wakiwa
wamepakizana kwenye pikipiki moja.
Alisema baada ya taarifa hizo
jeshi la polisi liliweza kufanikiwa kufika kijijini hapo mara tuu baada
ya muda mfupi na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa wote watatu wakiwa na
pikipiki hiyo ya marehemu Samweli waliompola baada ya kumuuwa.
Katika maojiano ya awali
bainiya jeshi la polisi na watuhumiwa hao watatu imeonyesha kuwa
watuhumiwa hao ndio waliohusika na mauwaji ya bodaboda huyo.
Kamanda Kidavashari ameleza watuhumiwa hao wote watatu wanatarajiwa kufikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamiliki.
![]() |
Picha jinsi alivyochinjwa) |
![]() |
via: wajanjawatown blogBOFYA HAPA LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK |
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment