Dunia haina huruma! Mtoto Samwel
Paulo (13), anayesoma darasa la nne Shule ya Msingi Amani wilayani
Ilala, Dar, amelazwa wodi ya watoto katika Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili, akiendelea kuuguza majeraha yaliyotokana na kile kinachodaiwa
ni kulipuliwa kwa moto na mama yake mzazi aliyetajwa kwa jina la
Doricus Iganga.
Kwa
upande wake, bibi yake, Helen Barnaba anayemuuguza mtoto huyo baada ya
mama yake kukamatwa na polisi alikuwa na haya ya kusema:
Tukio hilo la kusikitisha lilitokea
nyumbani kwao maeneo ya Mombasa Gongo la Mboto, Dar mwishoni mwa wiki
iliyopita, saa 8:00 usiku ambapo mwandishi wa habari hii alimtembelea
wodini hapo.
Alipoulizwa kisa na mkasa hadi kuwa katika hali mbaya kiasi hicho, mtoto huyo alikuwa na haya ya kusema:
“Najisikia vibaya sana kutokana na
maumivu makali ya moto. Sikutegemea kama mama yangu mzazi angenifanyia
hivi kwa kunituhumu kuwa nimemuibia fedha zake shilingi elfu kumi.
“Amekatisha ndoto yangu ya masomo, kwa sasa wenzangu wanajiandaa na mtihani wa muhula, mimi nipo wodini (huku akiangua kilio).
“Matukio kama haya huwa nimekuwa
nikiyasikia yakifanywa kwa watoto wenzangu kutoka kwa mama wa kambo na
siyo kwa mama mzazi kama ilivyotokea kwangu.
“Kwa hali hii hakuna mtu anayeweza kunionea huruma kama mzazi wangu hana uchungu na mimi.
“Sitegemei kuendelea kuishi na mama endapo Mungu akinisaidia nikapona.
“Ninachokikumbuka ni kwamba siku hiyo nilitoka shule, ilipofika saa 12:00 jioni, mama akawa amerudi kutoka katika kibarua chake.
“Alitupatia fedha ya kununua chipsi
kwa sababu alikuwa anaondoka kwenda kwenye shughuli yake nyingine ya
kuuza chakula maeneo ya Ukonga-Mazizini.
“Aliporudi usiku, mimi na mdogo wangu Salim Paulo (10), tulikuwa tumeshalala.
“Nakumbuka ilikuwa saa 8:00 usiku, mama alituamsha akawa anasema mimi na mdogo wangu tumemuibia fedha hasa mimi.
“Nilimkatalia kwamba sijachukua wala
sikujua alipoiweka, hakunisikiliza, alichukua mafuta ya taa na
kunimwagia kisha akanilipua na kutokomea kusikojulikana.
“Mdogo wangu alichukua maji kwenye ndoo na kunimwagia hadi moto ukazimika.
“Niliungua vibaya sana. Baada ya muda mfupi alirudi akijifanya yeye hahusiki, niliishiwa nguvu, nilipoteza fahamu.
“Nilikuja kujitambua nikiwa
hospitalini Amana. Hali ilikuwa mbaya ndipo nikaletwa hapa Muhimbili na
ninauguzwa na bibi yangu baada ya mama kukamatwa na polisi.
“Nawashukuru sana madaktari na wauguzi kwa kunihudumia kwa karibu.
“Nawashukuru sana madaktari na wauguzi kwa kunihudumia kwa karibu.
Naona mabadiliko kidogo ingawa tumbo linaniuma kwa ndani,” alisema mtoto huyo kwa masikitiko makubwa.
“Nikiwa kwangu Igunga, Tabora,
nilipigiwa simu kuwa mjukuu wangu kaunguzwa moto, nilizimia,
nilipozinduka nikaanza maandalizi ya kuja Dar.
“Nilipofika na kukuta hali kama hii, sikuamini kama mwanangu angeweza kufanya jambo kama hili.
“Hata hivyo, hii siyo bure bali ni mzunguko wa shetani, hawa wajukuu nilikuwa nikiishi nao kwa muda mrefu hadi pale nilipougua, nikamwambia mama yao awachukue.”
“Hata hivyo, hii siyo bure bali ni mzunguko wa shetani, hawa wajukuu nilikuwa nikiishi nao kwa muda mrefu hadi pale nilipougua, nikamwambia mama yao awachukue.”
Mtoto huyo kwa sasa yupo hospitalini
akiendelea na matibabu huku mama yake mzazi akishikiliwa kwenye Kituo
cha Polisi cha Sitaki-Shari, Dar kwa upelelezi ili sheria ichukue mkondo
wake.
Kwa yeyote atakayeguswa na kisa cha
mtoto Samwel, anaweza kufika katika wodi hiyo ya watoto au kuwasiliana
na bibi yake anayemuuguza kwa namba 0762 389774. Pia anaweza kumpatia
msaada wa fedha kwa namba hiyo, tunamuombea mtoto huyo apone ili
akajiunge na wanafunzi wenzake katika masomo.
>>>>>Credit GPL
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment