Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Mshairi, mtunzi na mwanaharakati Maya Angelou amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 86.

Alikuwa mmoja wa sauti za Marekani katika sekta ya uandishi. Alipata umaarufu mwaka 1969 baada ya kuandika kitabu kijulikanacho kama 'I Know Why the Caged Bird Sings' yaani 'Nafahamu Kwanini Ndege Waliofungiwa Tunduni Wanaimba'.

Ilikuwa ni moja kati ya vitabu saba ambavyo vimefuatilia maisha yake kuanzia utoto wake alipokuwa akinyanyaswa katika miaka ya 1930. Familia yake imesema "Aliishi maisha yake kama mwalimu, mwanaharakati, msanii, na mwanadamu. Alikuwa shujaa wa usawa, uvumilivu na amani."
Je umewahi kuona na kusoma kazi yoyote ya Maya? Tafadhali tuambie ukakumbuka kitu gani katika kazi zake.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top