Habari zimeenea nchini Afrika kusini kwamba Mwanariadha maarufu wa kike nchini humo Caster Semenya amejipatia mchumba wa kike.
Taarifa katika vyombo vya habari nchini humo zinasema kuwa mahari au
lobola kama inavyojulikana Afrika kusini imepelekwa kwa familia ya
mchumba huyo iliyoko Polokwane jimbo la Limpopo na zikakubaliwa kwa
mikono miwili na wazazi wa Violet Raseboya.
Aidha Lobola yaani mahari ya rand elfu 25 sawa na dola 2500 za Marekani ilikubaliwa kwa mikono miwili.
Hata hivyo Semenya mwenyewe anavilaumu vyombo vya habari kwa kuingilia maisha yake ya kibinafsi .
Mwandishi wa idhaa ya Kiswahili ya BBC nchini Afrika Kusini alipomtaka
kuthibitisha kama taarifa hizo ni za ukweli, Semenya alisema hatapinga
au kukubali
Vyombo vya habari nchini A-Kusini tayari vimeripoti kuwa Caster Semenya
(23 ) amekua na uhusiano wa kimapenzi kwa muda sasa na mwanariadha
mwenzie wa kike Violet Raseboya.
"Kama
unanijua vizuri basi unafahamu kuwa Caster hatangamani na vyombo vya
habari. Nakutana na waandishi wa habari wakati wa mashindano tu! Na wala
sitajishugulisha kujibu kama madai hayo ni kweli au la maanake ni swala
ambalo limechapishwa magazetini siwezi kubadili lolote!"
Mwanariadha huyo aliyegonga vichwa vya habari kote duniani mwaka wa 2009
alipompiku Janeth Jepkosgey wa Kenya na kutwaa ubingwa wa dunia wa mbio
za mita 800 za wanawake huko Berlin .
Wakenya walikata rufaa wakitilia shaka jinsia yake kutokana na maumbile yake yenye miraba minne.
Na matukio yaliyofwatia yalimlazimu Semenya kufanyiwa uchunguzi wa siha
na jinsia na shirikisho la riadha duniani IAAF jambo lililompa fedheha
sana bingwa huyo wa dunia.
Aliporejea nyumbani viongozi walioshabikia ushindi wake walimsifu kuwa
binti wa Afrika Kusini na hata magazeti ya urembo yakachapisha picha
zake akiwa amejipodoa .
Mwaka wa 2006 wakati wa utawala wa Thabo Mbeki serikali ya Afrika Kusini
ilipitisha sheria ya kuhalalisha mapenzi ya jinsia moja .
CHANZO:BBC SWAHILI
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment