STAA mkongwe wa vichekesho kutoka kundi la Kashikash Bongo Jessica Kindole ‘Safina’ akiwa hoi hospitali
=======
Safina ambaye ana ujauzito wa miezi 7, alifikishwa katika Hospitali
ya St. Monica iliyopo eneo la darajani, Manzese juzikati ambapo
alilazimika kulazwa baada ya madaktari kuona mwili wake umepoteza nguvu.
Kwa mujibu wa mtu aliyekuwa akimuuguza (hakupenda jina lake lichorwe
gazetini), staa huyo alipopimwa na daktari, aligundua kuwa ana ugonjwa
wa UTI pamoja na ugonjwa huo wa kuendesha damu huku ndugu zake
wakimuombea usiku na mchana.
Baada ya waandishi wetu kuzinyaka taarifa hizo, walimpigia simu staa
huyo ambapo alipopatikana alisema anamshukuru Mungu anaendelea vizuri
na kudai alikuwa anasumbuliwa na malaria pamoja na kutapika.
“Nashukuru kwa kunijulia hali, sasa naendelea vizuri na mtoto anaendelea vizuri namshukuru Mungu,” alisema Safina.
Nesi mmoja ambaye pia hakupenda jina lake liandikwe gazetini,
aliwaambia waandishi wetu kuwa mtoto aliye tumboni alikuwa hachezi kwa
muda mrefu lakini mpaka tunakwenda mtamboni, alikuwa akiendelea vizuri.
Imeandikwa na Hamida Hassan na Gladness Mallya, GPL.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment