Inspector
Henry akiwasihi mahabusu hao wawili wanaotuhumiwa kwa kesi za mauaji, kuachia
mlingoti wa Bendera ya Taifa na kurudi kwenye chumba cha mahakama kwaajiri ya
taratibu za kesi.
|
....................Ushawishi
ukiendelea............................
|
Mahabusu
Thobiasi Warioba (aliye mtupu) pamoja na mwenzake Hamis Ramadhani katu katu
waking'ang'ania mlingoti wa bendera ya Taifa huku wakishinikiza kuzungumza na
waandishi wa Habari.
|
..........Wananchi
wamefurika viwanja vya mahakama kushuhudia tukio hilo la Mei 07,2014..........
|
Baada ya
kuzungumza na waandishi wa habari mahabusu hao walikubali kurejea chumba cha
Mahakama.
|
..........Wananchi wamefurika viwanja vya mahakama kushuhudia tukio hilo la Mei 07,2014.......... |
Mahabusu
wawili kati ya Sita wanaotuhumiwa kwa kesi za mauaji, wameleta kizaazaa baada
ya kujaribu kutoroka na kukimbilia kwenye mlingoti wa Bendera ya Taifa na kuing'ang'ania
kisha kuvua nguo na mmoja wao kubaki mtupu.
Tukio hilo
limetokea Mei 07,2014, majira ya saa 4:00 asubuhi katika Mahakama ya Hakimu
Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza, wakati mahabusu hao
walipofikishwa kwa ajili ya kusikilizwa kwa kesi zao, lakini ghafla walipofika
kwenye viwanja vya mahakama hiyo walitimua mbiyo kuelekea kwenye mlingoti wa
Bendera hiyo ya Taifa na kuvua nguo.
Wananchi
waliokuwa katika viwanja vya mahakamani hapo waliachwa midomo wazi na hali ya
mshangao, mara baada ya mmoja kati ya hao wawili wakifanikiwa kuufikia mlingoti
huo na kuvua nguo kisha kuanza kupiga kelele kwa kupaza sauti kudai haki
itendeke.
Tukio hilo
pia lilishuhudiwa na watumishi wa Mahakama ya Wilaya, Mahakama ya Mwanzo,
Mamlaka ya Maji Safi na Majitaka ya jijini hapa (MWAUWASA), Askari wa Jeshi la
Wananchi (JWTZ), na taasisi zingine zilizo jirani na majengo ya mahakamani hapo
na wananchi waliokuwa wakisubilia kesi zao kutajwa.
Mahabusu hao
sita waliojaribu kutoroka na kuishia kudhibitiwa vyombo vya dola, walitajwa kwa
majina kuwa ni Thobiasi Warioba (35), aliyeamua kuvua nguo zote na kubaki mtupu
eneo la mlingoti wa Bendera ya Taifa, ambaye anakabiliwa na kesi ya mauaji Na.
32/2012.
Watuhumiwa
wengine waliojaribu kutoroka ni Hamis Ramadani (30), Anthony Petro (35), Marwa
Mwita (38), na Chacha Wangwe (35), na mwingine ambaye hakufahamika majina yake
mara moja, wote wanakabiliwa na kesi ya Jinai Na. 215/2013 na walikamatwa tangu mwaka 2011.
Wakiwa
katika viwanja vya mahakama hiyo baada ya kudhibitiwa na askari polisi, mmoja
wa mahabusu hao walisikika wakisema: “Haiwezekani, tangu mwaka 2011
tulipokamatwa hadi sasa kesi zetu hazijasikilizwa.
Wengine
tumebambikiziwa kesi. … “Tunaomba haki zetu, polisi mnatuonea, vyombo vya
habari tunaomba mtusaidie tumekaa muda
mrefu bila kusikilizwa na hatujui hatma yetu tangu 2011 tulipo kamatwa
tumechoka kukaa mahabusu, tunaomba kesi zetu zisikilizwe”.
Baada ya
malalamiko yao, ndipo askari mmoja
aliyejitambulisha kuwa ni Inspekta Henry akiwa na wenzake sita waliokuwa
wakiwadhibiti wasikimbie na kuwahoji kuhusiana na madai yao, huku askari hao
wakiwataka kuondoka katika mlingoti huo na kumtaka Warioba avae nguo ili waweze
kuingia mahakamani.
“Pamoja na
maamuzi yenu haya, lakini mtambue mnavunja sheria na hili ni kosa jingine la
jinai, hivyo ni vema mkaondoka kwenye mlingoti huu na kuingia mahakamani.
Malalamiko yenu tumeyasikia na yatashughulikiwa,” alisema Inspekta Henry.
Mmoja wa
maofisa waandamizi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza, ambaye alikataa
kutajwa jina lake, alidai ushahidi wa kesi za watuhumiwa hao bado
haujakamilika, na kwamba kesi zao haziwezi kusikilizwa na mahakama ya wilaya
kwani haina uwezo na badala yake zitatajwa tu kisha kuhamishiwa Mahakama Kuu.
“Bado hiyo
ni Criminal Case (kesi ya mauaji) au PI Case hivyo Mahakama Kuu haiwezi
kuzungumzia hilo kwa sasa kwa kuwa utaratibu wa mahakama kuu ikisha kuwa tayari
huitwa ‘Criminary Session Case’, ambapo sasa hupangiwa namba ya kesi na Jaji wa
kuisikiliza,” alisema.
Picha/Habari
Na:-Gsengo Blog.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment