Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Belle 9 ni miongoni mwa wasanii wakali nchini ambao hawajawahi kuwa na bahati na tuzo za Kilimanjaro na mwaka huu bahati haikuwa kwake pia. Kukosa kwake tuzo kumewaumiza mashabiki wake akiwemo Elizabeth Michael aka Lulu.

Kupitia Twitter, Lulu ameandika:
Namshukuru Mungu kwa ushindi wa @FidQ sasa mwaka mtakaompa Tuzo Belle 9 nitatoa sadaka kabisaaaaa." Lulu akimkabidhi tuzo Vanessa Mdee kwenye usiku wa KTMA weekend iliyopita
Kauli ya Lulu imempa moyo Belle 9 ambaye ameiambia Bongo5: "Nachoweza kusema hapo Lulu kuna kitu amekiona kwenye muziki wangu ndio maana akasema kauli hiyo. Hii inanipa nguvu zaidi ya kuongeza juhudi zaidi kwa kile ninachokifanya ili nifike mbali zaidi. Kama Lulu kasema hivyo hebu jiulize ni wangapi? Wanatambani kitu kama hicho,kwahiyo ni dhahiri kuna watu wengi sana wanafuatilia muziki wangu.
Chanzo:bongo5

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top