Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Msanii wa muziki na producer wa Sharobaro Record, Bob Junior amekanusha habari zilizoandikwa na gazeti la udaku la Maskani kuwa anamloga Diamond. 

bob Amesema hawezi KUfanya kitu kama hicho na Diamond atabaki kama Diamond na yeye kama yeye. 
"Niupu....vu kuandika kitu kama hicho, nani mambo ya ki..nge,mimi nimekasirika sana,huwezi andika kitu kama hicho. Hivi mimi naweza nikamloga Diamond,unajua Diamond atabaki kuwa Diamond na Bob Junior atabaki kama Bob Junior,huu wote ni uongo tu,sipendi kuyaongelea haya mambo na sina tatizo na mtu yoyote," amesema. Pia Bob Junior alizungumzia tuhuma za kuhusisha muziki wake na waganga wa kienyeji. 
 bob
"Sijawai kujihusisha na masuala ya waganga,mimi nimelelewa katika familia ambayo hata simjui mganga. Nashukuru Mungu toka nimezaliwa mpaka hapa. 
Sehemu kubwa yaani nasaidiwa na wazazi wangu vizuri mpaka ikafika wakati najitegemea mwenyewe. 

Kwahiyo sijui chochote kuhusu suala la mganga."

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top