Msichana huyo aliyebakwa aonekanavyo kwa karibu zaidi.
DUNIA ina maajabu jamani! Msichana wa miaka 14 (jina limehifadhiwa)
amebakwa huku mwenzake aitwaye Mecy (11) akipigwa na kuporwa simu na mtu
aliyedai kuwa ni askari polisi (kituo hakijulikani).
Kwa mujibu wa Mecy (pichani)ambaye ni mkazi wa Kinondoni Msiriri jijini Dar, tukio hilo lilijiri hivi karibuni ambapo wote walijikuta wakipata dhahama hiyo baada ya kukutana na afande huyo na kuwafanyia vitendo vya kinyama.
Msichana
wa miaka 14 (jina limehifadhiwa) kushoto aliyebakwa huku mwenzake
aitwaye Mecy (11) akipigwa na kuporwa simu na mtu aliyedai kuwa ni
askari polisi (kituo hakijulikani).
Akizungumza na Uwazi, Mecy ambaye alipigwa na kuporwa simu alisema:
“Ilikuwa saa kumi jioni, mimi nikiwa natembea njiani nilikutana na mwanaume aliyenisimamisha na kusema yeye ni polisi. Alidai mimi ni mzururaji, baadaye akasema nimemtukana, akaniambia tuongozane kwenda kituo cha polisi.
“Tukiwa njiani, alianza kunipiga sana na kunipora simu kisha
akanifunga pingu. Mbele tulikutana na rafiki yangu (anayedaiwa kubakwa
mkazi wa Kinondoni- Shamba) naye akaunganishwa katika msafara,” alisema
Mecy.
Mecy aliendelea kusema: “Tuliendelea kuzungushwa na yule polisi kuanzia hiyo saa kumi jioni hadi giza likaanza kuingia.
“Tulifika sehemu akatupeleka kichochoroni, wakati huo mimi nikiwa
bado na pingu. Akaniweka Kwenye kona ya nyumba na kwenda kumbaka
mwenzangu.“Baada ya kumaliza akasema ile ndiyo ilikuwa adhabu ya
mwenzangu, mimi adhabu yangu ni kile kipigo na kunipora simu.”
Baada ya simulizi ya Mecy, mwandishi wetu alifanikiwa kuzungumza na anayedai kubakwa, alikiri kufanyiwa kitendo hicho, akasema:
“Nilikutana na (anamtaja jina) akiwa na huyo mwanaume ambaye kweli
alimpiga na kumpora simu ila sikumuona kama alimfunga pingu, nadhani kwa
sababu ya kitete nilichokuwa nacho.”
Mwenyekiti wa Mtaa wa Msisiri A, Omar Muhunzi alikiri kupata taarifa hizo za binti hao kufanyiwa kitu mbaya.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Msisiri A, Omar Muhunzi alikiri kupata taarifa hizo za binti hao kufanyiwa kitu mbaya.
Alisema baada ya tukio, mabinti hao walikwenda kuripoti Kituo cha
Polisi cha Msisiri na kupewa PF3 yenye namba ya jalada MSR/RB/255/2014
KUCHUNGUZWA KAMA AMEBAKWA.
Kwa mujibu wa maelezo ya mama yake mdogo wa anayedai kubakwa, binti
huyo alipelekwa Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar ambako alilazwa kwa
siku mbili na kupimwa akitakiwa kurudi tena baada ya mwezi mmoja.
“Kwa sasa tunaelekea Kituo cha Polisi Oysterbay kwa ajili ya kufuatilia ili haki itendeke,’’ alisema mama huyo.
CREDITS: UWAZI
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro








Post a Comment
Post a Comment