Rais Jakaya Kikwete alipomtembelea kumjulia hali bilionea
kijana anayemiliki kampuni ya uuzaji na usambazaji wa vifaa vya
nyumbani ya Home Shopping Centre ya Kariakoo jijini Dar es Salaam, Said
Saad Mohamed .
KUNA madai mazito kwamba, yule bilionea kijana
anayemiliki kampuni ya uuzaji na usambazaji wa vifaa vya nyumbani ya
Home Shopping Centre ya Kariakoo jijini Dar es Salaam, Said Saad Mohamed
amehama Bongo baada ya lile tukio la kikatili la kumwagiwa tindikali
lililotokea mwaka jana maeneo ya Msasani, Dar.
Habari za uhakika kutoka chanzo makini ambacho pia kipo karibu na
familia hiyo ya kitajiri zinasema baada ya kukamilika kwa matibabu yake
yaliyoanzia nchini Afrika Kusini na baadaye Ujerumani na kupona,
mfanyabiashara huyo aliamua kuhamishia maskani yake kwenye Jiji la Dubai
ambao ni mji mkuu wa Muungano wa Nchi za Kiarabu (United Arab
Emirates).
Kule inasemekana bilionea huyo licha ya kuwa na biashara anamiliki nyumba.
KISIKIE CHANZO CHETU
“Said hakai tena hapa Bongo, amehama yeye na familia yake, hivi sasa anaishi Dubai. Unajua anaogopa kuendelea kuishi hapa baada ya lile tukio, ameona anaweza kuuawa maana hajui nani ni adui nani rafiki, huwa anakuja mara mojamoja, anakaa siku mbili tatu anaondoka zake,” kilisema chanzo hicho.

NI UAMUZI WA FAMILIA
Inadaiwa kuwa baada ya kutibiwa Afrika Kusini na kisha Ujerumani ambako alifanyiwa upasuaji wa mafanikio wa macho yaliyokuwa yameathiriwa na tindikali hiyo, familia ilikaa chini na kuamua kwamba ndugu yao asikae tena Tanzania.

“Kama suala ni biashara, hata Dubai ana biashara, tena kubwa tu, sasa
kwa nini asikae huko ambako ni salama kuliko hapa? Kule ana nyumba
nzuri na maisha ni mazuri, jamaa hawezi tena kurudi na kuishi hapa,
kimsingi amehama kimoja,” kilisema chanzo hicho.
Jitihada za kumpata bilionea huyo kupitia namba zake za simu za siku
za nyuma zilishindikana, kwani zote hazikuwa hewani, lakini mtu mmoja wa
karibu na familia hiyo maarufu zaidi Kariakoo, alithibitisha kuhama kwa
mfanyabiashara huyo, Mtanzania mwenye asili ya Yemen.
KUMPATA MSEMAJI WA FAMILIA NI KAZI KUBWA
Uchunguzi zaidi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa, usiri umetawala kwenye familia ya bilionea huyo ambapo kumpata msemaji imekuwa kazi kubwa.
Uchunguzi zaidi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa, usiri umetawala kwenye familia ya bilionea huyo ambapo kumpata msemaji imekuwa kazi kubwa.
“Unajua yaliyotokea ndiyo yametoa fundisho, huwezi kumpata mtu
akasema chochote kuhusu Said kwani kila mtu anaogopa, maana unaweza
kusema huyu ni rafiki kumbe ni adui mkubwa,” kilisema chanzo.
MTUHUMIWA BADO KUKAMATWA
Kwa mujibu wa Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi, Kinondoni, Dar es Salaam, ACP Camillius Wambura alisema juzi kwamba mpaka sasa hawajafanikiwa kumpata mtuhumiwa.
“Kusema kweli sina taarifa kama kuna mtu aliyekwishakamatwa kuhusiana na kummwagia tindikali huyo bwana,” alisema Wambura.

TUJIKUMBUSHE
Said alimwagiwa tindikali Julai 19, mwaka huu, mishale ya saa 2 usiku akiwa kwenye moja ya maduka yake yaliyopo kwenye jengo analodaiwa kulimiliki la Msasani Mall jijini Dar es Salaam.
Ilielezwa kuwa baada ya kumwagiwa tindikali alikimbizwa kwenye Hospitali ya Ami Wellness Centre iliyopo Masaki, Dar lakini ndani ya kipindi kisichozidi dakika 60 alichukuliwa na kupandishwa ndege kupelekwa nchini Afrika Kusini.

“Sehemu ya usoni kushuka kifuani upande wa kulia na mkono wenyewe wa
kulia ndiyo maeneo katika mwili wa ndugu yetu yaliyoathirika zaidi na
tindikali,” alisema ndugu huyo wa ndani kabisa kwa sharti la kutotajwa
jina, akaongeza:
“Jicho la kulia lenyewe lilipata athari kidogo, kwani inaonekana
wakati mmwagaji akifanya kile kitendo, yeye alifumba macho kwa hiyo
tindikali haikuingia ndani ya jicho.
“Ila kwa vile tindikali ilimwagika kwa wingi juu kwenye jicho la
kulia na kutokana na ukali wa tindikali aliyomwagiwa, imesababisha
kutengenezwa kwa mtoto wa jicho kwa hiyo hawezi kuona mbali.
“Uamuzi wa kumpeleka Ujerumani ulifikiwa baada ya kujiridhisha kwamba
kule kuna wataalamu kuliko Afrika Kusini. Oparesheni ya uso kubadili
ngozi iliyoathirika, vilevile kufanya upasuaji wa jicho na kuliweka sawa
ni mambo ambayo tulijiridhisha yanawezekana Ujerumani.”
NYUMBANI KWAKE KARIAKOO
Juzi, Uwazi lilifunga safari hadi kwenye nyumba ya bilionea huyo, Kariakoo lakini hakukuwa na ushirikiano wowote kutoka kwa mtu aliyedai ni mlinzi wa nyumba hiyo.
Juzi, Uwazi lilifunga safari hadi kwenye nyumba ya bilionea huyo, Kariakoo lakini hakukuwa na ushirikiano wowote kutoka kwa mtu aliyedai ni mlinzi wa nyumba hiyo.
CHANZO: UWAZI
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro

Post a Comment
Post a Comment