KWA mara nyingine, staa wa sinema za
Kibongo, Yobnesh Yusuf ‘Batuli’ amemwaga data za kimapenzi akidai
hajawahi kumpenda mwanaume kama alivyompenda Nice Mohammed ‘Mtunis’.
Akizungumza na paparazi wetu hivi
karibuni, Batuli alisema licha ya kuwa walimwagana na staa huyo lakini
hatokuja kupenda mwanaume kama alivyompenda Mtunis.
“Nilivyompenda Mtunis ni ngumu sana
kumpenda mwanaume mwingine kama hivyo na kwa kawaida kupenda huwa ni
mara moja tu mengine tutadanganyana,” alisema Batuli.
Hivi karibuni Batuli aliripotiwa
kutikisa ndoa ya Mtunis ikidaiwa kuwa bado ana uhusiano naye lakini cha
ajabu mtoto wa kike hakuonesha dalili zozote za kukanusha taarifa hizo.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment