Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Balozi wa Malawi nchini Tanzania Mhe.
Flossy Gomile-Chidyaonga (picha chini)
amefariki dunia leo jijini Dar es salaam
baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Ni kwa masikitiko makubwa Wizara ya
Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa (ya Malawi) unauarifu umma
kufariki dunia kwa Balozi Flossy
Gomile-Chidyaonga baada ya kuugua kwa
muda mfupi jijini Dar es salaam
mchana huu”, imesema taarifa iliyotolewa na
msemaji wa Wizara hiyo Quent Kalichero.
Tangu mwaka 2006 Marehemu Bi Flossy
Gomile-Chidyaonga alikuwa
Naibu Balozi wa Malawi London kabla ya
kuteuliwa kuwa Balozi wa Malawi
nchini Tanzania mnamo Septemba mwaka
2011”, imesema taarifa hiyo na kuongezea
kuwa taratibu za mazishi zitatangazwa baada
ya taratibu kukamilika.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top