Basi
la abiria mali ya kampuni ya CHAKITO LONG WAY namba T354 ARK
linalofanya safari zake kati ya jiji la Arusha na jiji la Dar es salaam
limemgonga mtoto aliyekuwa akiendesha baiskeli na kumuua palepale baada
ya kumuumiza vibaya wilayani Korogwe. Kwa mujibu wa shuhuda wetu mtoto
huyo amegongwa na basi hilo alipokuwa akivuka barabara na basi hilo
ambalo lilikuwa katika mwendowa kasi kuelekea jijini Dar es salaam.
Maiti ya kijana huyo ambaye hakufahamika jina lake mara moja
Katika ajari nyingine zaidi ya
abiria 50 waliokuwa wakisafiri na basi la MAJINJAH SPECIAL ambalo
hufanya safari zake kati ya mikoa ya Dar es salaam na Mbeya
wamenususrika kufa baada ya basi lao kuacha njia na kwenda kutumbukia
katika korongo mjini Iringa maeneo ya Mafing leo asubuhi lilipokuwa
likiktokea mjini Mbeya kuelekea jijini Dar es salaam . Ajari hiyo
imetokea asubuhi ya leo na chanzo chake ni kufeli kwa breki katika basi
hilo.
Kwa mujibu wa shuhuda wetu hakuna
aliyepoteza maisha katika ajari hiyo na basi lilitolewa na kuendelea na
safari yake ya Dar es salaam.
<<<<Bofya hapa ulike page yetu>>>>
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro












Post a Comment
Post a Comment