
Mwenyekiti
wa Kamati namba tatu ya Bunge Maalumu la Katiba, Shamsi Vuai Nahodha
akiongoza mjadala wa kikao cha kamati hiyo mjini Dodoma jana. Kulia ni
mjumbe wa kamati hiyo, Anne Makinda. Picha na BMK
Dodoma.
Bunge la Katiba jana lilianza kujadili Rasimu ya Katiba kwa misukosuko
kwenye Kamati baada ya kuvamiwa na kundi la wanaharakati waliokuwa na
mabango wakidai hati halisi ya Muungano yenye saini za Mwalimu Julius
Nyerere na Abeid Karume.
Msukosuko
mwingine uliozikumba karibu kamati zote zinazoanza kujadili rasimu hiyo
kwa kuanzia sura mbili zinazohusu Muungano – sura ya kwanza na ya sita
na kuzua malumbano, ni maana ya maneno dola, shirikisho, muungano na
nchi.
Wakati
waandamanaji wenye mabango wakiishia mikononi mwa polisi, suala la
Muungano lilitulizwa kwa kuitwa wanasheria kutoa tafsiri sahihi kwa kila
neno.
Katika
kamati zote, suala la muda wa kamati kujadili sura hizo mbili kwa siku
mbili kila moja pia liliibua mjadala mkali, hadi kuwalazimisha baadhi ya
wenyeviti wa kamati kuamua kumwandikia mwenyekiti wa Bunge, Samuel
Sitta kuomba muda uongezwe.
Hali hiyo
imejitokeza Bunge hilo likiwa limeshakaa siku 40 kabla ya kuingia
katika mjadala rasmi, baada ya kupoteza muda mwingi katika kutengeneza
kanuni za uendeshaji wa chombo hicho.
Wanaharakati wavamia
Wakati
kamati zikijiandaa kuanza mjadala, wanaharakati wawili walivamia kwenye
ukumbi wa Royal Village, wakiwa na mabango yenye maandishi yanayowataka
wajumbe kutetea maoni ya wananchi yaliyomo kwenye rasimu ya Katiba.
Hata hivyo, watu hao baadaye waliondolewa kwenye eneo la hoteli hiyo na maofisa wa usalama majira ya saa 2:00 asubuhi.
Hata
hivyo, mwenyekiti wa Kamati Namba 9, ambayo inafanya vikao vyake kwenye
hoteli hiyo, Kidawa Hamis alisema kuwa hali ni shwari kwenye kamati yake
na wajumbe wanaendelea kuchambua rasimu.
Katika
kumbi zilizopo kwenye Hoteli ya St. Gasper, pia watu wawili walikamatwa
wakiwa na mabango yanayowataka wajumbe kutambua kwamba katiba ni mali ya
wananchi na si ya wanasiasa.
Hati ya Muungano
Katika
makundi karibu yote, jana kuliibuka hoja juu ya Hati ya Muungano,
wajumbe wakitaka kabla ya kuanza mjadala ionyeshwe kwa kuwa ndio msingi
wa hoja.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment