Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Michuano ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara
msimu wa 2013/14 imefikia tamati leo
(Aprili 19, 2014) kwa timu zote 14 kuwa
viwanjani, na kushuhudia Ashanti United
ikiteremka daraja kurudi ligi ya daraja la
kwanza msimu ujao.
Ashanti United iliyopanda daraja katika
msimu huu unaomalizika, imefungwa na
Prisons ya Mbeya bao 1-0 katika mchezo
wa funga dimba uliopigwa leo katika
uwanja wa Jamhuri morogoro.
Katika Mechi hiyo Ashanti ilikuwa
ikitakiwa kupata ushindi wa aina yoyote
ili kuiacha Prisons ambayo ilikuwa
ikilingana nayo point (25).
Kwa matokeo hayo Prisons imefikisha
point 28 na kuiacha Ashanti ikiunga na
timu za Rhino Rangers na Oljoro JKT.
Mabingwa wapya Azam waliokabidhiwa
kombe lao leo katika uwanja wa Azam
Complex, Dar es Salaam wamenogesha
sherehe zao kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi
ya JKT Ruvu, na hivyo kumaliza ligi
wakiwa na point 62, wakiwa
hawajapoteza mchezo hata mmoja.
Katika mchezo uliowakutanisha watani wa
jadi Yanga na Simba uwanja wa Taifa
DSM, matokeo ni kwamba timu hizo
zimetoshana nguvu kwa kufungana bao
1-1 katika mchezo uliokuwa na vioja vya
hapa na pale.
Simba ndiyo walikuwa wa kwanza kupata
bao kupitia kwa Haruna Chanongo dakika
ya 76 kabla ya Simon Msuva kuisawazishia
Yanga katika dakika ya 86.
Katika hali ya kushangaza, Baadhi ya
wachezaji wa Yanga wakiongozwa na
Didier kavumbagu, walivamia na
kuliondoa golini taulo la Golikipa wa
Simba Ivo Mapunda kwa madai kuwa
linachangia kukosekana kwa magoli.
Baada ya kavumbagu kuliondoa taulo hilo,
palizuka tafrani ndogo iliyosababisha
mpira kusimama kwa dakika kadhaa
kabla ya Ivo Mapunda kupewa taulo
lingine na mchezo kuendelea huku Didier
kavumbagu akizawadiwa kadi ya njano.
Pasipo kufahamu alitokea wapi, shabiki
mmoja wa Yanga alishuka dimbani na
kuliondoa taulo lile na kukimbia nalo
jukwaani kabla ya kudhibitiwa na askari.
Kwa matokeo hayo Yanga imemaliza ligi
ikiwa nafasi ya pili na point 56 wakati
Simba wakiwa nafasi ya 4 na point 38,
sawa na Kagera Sugar, lakini ikiizidi
tofauti ya magoli.
Matokeo ya mechi nyingine zilizopigwa
leo ni kwamba Rhino Rangers imefungwa
mabao 2-0 na Ruvu Shooting (Uwanja wa
Ali Hassan Mwinyi, Tabora), Mbeya City
imeifunga Mgambo Shooting bao 1-0
katika Uwanja wa Sokoine, Mbeya, Oljoro
JKT na Mtibwa Sugar zimetoka sare ya
bao 1-1 katika Uwanja wa Sheikh Kaluta
Amri Abeid, Arusha na Coastal Union
imechezea kipigo cha bao 1-0 toka kwa
Kagera Sugar katika uwanja Mkwakwani,
Tanga.

kikosi cha ashanti.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top