Akizungumza
na mwandishi wa habari ,March 31,2014,wodi namba 5 katika hospitali ya Rufaa ya
Maweni, mwanafunzi huyo aliyetambuliwa kwa jina la Zubeda Athuman (14)
alisema chanzo cha mwalimu huyo kumchukia na hatimaye kufikia hatua ya
kumpiga na kumvunja mguu ni wivu wa kukataliwa kupewa penzi ,hali iliyomfanya
mwalimu huyo kumpa adhabu za hapa na pale kila aendapo shule.
Hali hiyo
ilimfanya mwanafunzi huyo kuwadokeza wazazi wake ambapo walimwambia
avumilie,ndipo Jumatano ya wiki hii mwalimu alimpa adhabu ya kuchimba shimo na
alikataa kufanya hivyo baada ya kuona hana kosa la msingi la kumpa adhabu hiyo.
Mwalimu huyo
alifikia hatua ya kumfuata nyumbani kwao machi,22,2014 saa 12.30 jioni
hali iliyowashtua wazazi na kumuhoji mtoto juu ya hilo ndipo binti alipokwenda
shule Machi,24,2014 alimuliza mwalimu huyo sababu ya kumfuta kwao, hali
hiyo ilimchefua mwalimu na kutoa maneno ya kashfa na kumpiga vibao
vya uso na kusababisha maumivu mbalimbali ya mwili wake ikiwemo kuvunjika kwa
mguu.
Mganga Mkuu
wa Hospitali ya Maweni, Macris Yakayeshi ,amekiri mwanafunzi huyo kuvunjika
mguu wa kulia sambamba na kuvimba uso na kupelekea mdomo kwenda upande na wiki
ijayo anatarajia kumwekea `P.O.P’.
Dr.Yakayeshi
alibainisha kuwa kutokana na tatizo alilonalo itamlazimu kukaa na mhogo si
chini ya wiki sita ili mguu utengamae sambamba na kuitaka jamii ibadilike na
matukio ya udhalilishaji wa kijijnsia huku akidai alifikishwa hapo kifua kikiwa
wazi ili hali binti ni rika la balehe na kuomba sheria ichukue mkondo wake.
Mwenyekiti
wa Mtaa wa Kamala katani humo Curthbert Kusongwa alisema, kwa maelezo
aliyoyapata kutoka kwa walimu wa shule hiyo walidai binti alikataa adhabu
aliyopewa na kumpiga kofi mwalimu na ndipo mwalimu akamwambia akamlete mzazi
wake,wazazi walipofika alidai alimvamia mwalimu na kuanza kumpiga hali iliyolazimu
jeshi la polisi kuingilia hekaheka kiyo.
Akizungumzia
tukio hilo Athumani Moshi ambaye ni baba wa Zubeda alisema alishangaa
kumuona mwanae amerudishwa shule huku akiwa amevimba uso na mdomo ndipo akadai
kuitwa na mwalimu husika,alipofika shule na kuonana na mwalimu husika hakuwa
muungwana kutokana na kauli chafu na kebehi.
Moshi
alisema baada ya kauli hizo ghafla mwalimu akamkata mtama mwanae na
kuanguka chini ndipo wakapigana,huku akikiri awali alipata kuelezwa juu ya adha
ya mwalimu huyo kwa binti yake hadi kufikia hatua ya kumfuata usiku siku za
mapumziko sanjari na kumpa adhabu zisizostahili kwa kisa alikataa kuwa nae
kimapenzi.
Kamanda wa
polisi mkoani Kigoma Kamishina Msaidizi Freisser Kashai amesema Jeshi la polisi
mkoani Kigoma linamshikilia Mwalimu huyo,Alcado Kigona wa shule ya Msingi Bangwe
kwa tuhuma za kumshambulia mwanafunzi wake na kumvunja Mguu na kwamba uchunguzi
wa awali unaonesha kuwa mwalimu huyo alikuwa akimtaka kimapenzi mwanafunzi huyo
na kwamba Uchunguzi bado unaendelea na kwamba mtuhumiwa atafikishwa mahakamani
wakati wowote baada ya uchunguzi kukamilika.
Kwa nyakati
tofauti Mariamu Issa na Winyfrida Bwire walisema sheria ya mwanafunzi juu ya
adhabu inajulikana ,walimu hawana budi kulea watoto kwa kuwafundisha adabu
,huku wakidai kuna namna kati ya mwanafunzi na mwalimu haiwezekani kukataa kwa
adhabu amvunje mguu.
Habari Na:-Magreth
Magosso-Kigoma.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment