Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Afrika Kusini ni nchi yenye uchumi mkubwa Afrika ambao umevutia Waafrika wengi kukimbilia huko kwa ajili ya kufanya kazi kama za Udereva, uuzaji mafuta kwenye vituo vya mafuta pamoja na kazi nyingine mbalimbali.
Taarifa kutoka kwenye mji wa Pretoria ni kwamba Watanzania ambao wanamiliki na kufanya biashara mbalimbali zikiwemo za Maduka na wale wanaomiliki hoteli, wamevamiwa wakiwa kwenye mali zao na kufanyiwa uharibifu na nyingine kuchomwa moto.

Ni kundi la watu ambalo linaendeleza uvamizi huu ambapo linawashutumu Watanzania hawa kuhusika na biashara ya dawa za kulevya, yani kwa ufupi Watanzania wanasema hata kama kweli wangekua wanafanya hii biashara, walio na mamlaka ya kuwavamia ni Polisi na sio hao raia.

Inaaminika kundi hili lina sehemu kubwa ya madereva Taxi wazawa wa nchi hiyo ambao wamekua wakiumizwa na jitihada za raia wa kigeni wa Nigeria na Watanzania ambao wamejazana kwenye mtaa wao wakimiliki maduka mbalimbali yakiwemo ya nguo pamoja na hoteli.
 
Tayari balozi wa Tanzania amekutana na Watanzania hao na kuahidi kulifatilia ambapo ni Watanzania watano wamejeruhiwa wakiwemo watatu ambao bado wako hospitali na mmoja wao kavunjika mkono, mmoja kapigwa kichwani.
 
Kabla ya Watanzania wengine kuwahi kufunga maduka yao, maduka matatu ya Watanzania pamoja na hoteli mbili zinazomilikiwa na Watanzania zilivamiwa na wakachuchukuliwa simu na watu kupigwa ambapo polisi walipokuja hakuna chochote kilichofanyika zaidi ya maelezo.
Picha hizi zote zilipigwa na Mtanzania akiwa anakimbia baada ya kufanikiwa kufunga duka lake

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top