
Matumaini aliyosalia nayo mwanamume huyo ni ya kwenda mbinguni
Mwanamume mmoja nchini Kenya
aliwaacha wakazi wa kijiji cha Tivani mkoa wa Bonde la uffa vinywa wazi
baada ya kujichimbia kaburi na hata kujaribu kujizika mwenyewe kutokana
na alichosema ni matatizo ya ndoa.
Kwa mujibu wa kituo cha runinga cha KTN nchini
Kenya, tukio hilo lililotokea Jumanne asubuhi na kuwashangaza wakazi wa
eneo la Trans Nzoia mkoa wa Rift Valley
Mwanamume huyo, alidai kuwa ana
matatizo ya ndoa ambayo yeye mwenyewe ameshidwa kuyatatua na kwa hivyo
kwake kilichosalia ni kwenda mbinguni.
Alisema mkewe alikuwa amemwambia jambo ambalo lilimkera roho na ndhio maana akaamua kujitoa uhai.
Mwanamume huyo kwa jina Kipsang , alichimba
kaburi hilo usiku na hata kujaribu kujizika akiwa hai wakati mkewe na
watoto wake walipokuwa wanalala.
Wanakijiji katika kijiji cha Tivani walikuwa na
wasiwasi kuwa mwanamume huyo alikuwa amerukwa na akili ingawa walikiri
kwamba yeye na mkewe wamekuwa wakikumwba na matatizo ya ndoa.
Mkewe alisema kuwa amechoshwa na mwanamume huyo ambaye ametelekeza familia na majukumu yake.
Baba huyo wa watoto wawili ambaye ni kondakta wa
matatu, hatimaye aliondoka katika kaburi hilo baada ya wanakijiji
kumsihi huku wazee wakiwataka watu kupanda migomba ya Ndizi neneo
alilokuwa amechimba kaburi hilo ili kuzuia mikosi.
>>>>>>Chanzo bbcswahili
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment