
Watu 25 walijeruhiwa vibaya katika shambulizi hilo lililotokea Jumatatu usiku
Polisi nchini kenya wanasema
kuwa wamewakamata zaidi ya watu 200 kufuatia mashambulizi ya hapo jana
Jijni nairobi ambapo takriban watu sita waliuawa.
Wengine 25 walijeruhiwa katika mashambulizi hayo
matatu yaliotokea kwa wakati mmoja katika mtaa wa Eastleigh ambapo raia
wengi wa kisomali wanaishi na kufanya kazi.
Polisi wanasema kuwa milipuko hiyo iliyotokea
katika mikahawa miwili midogo huenda ilisababishwa na magurunedi pamoja
na mabomu la kujitengezea.
Kumekuwa na mashambulizi kadhaa mjini Nairobi
pamoja na mjini Mombasa katika miezi ya hivi karibuni ,ambapo polisi
wanawalaumu waislamu wenye itikadi kali.
chanzo bbcswahili
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment